Hebrews 7:26 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, ilikuwa jambo la kufaa sana kwetu kuwa na kuhani kama huyo, mtakatifu, asiye na hatia wala dhambi ndani yake; ametenganishwa mbali na wenye dhambi, na ameinuliwa juu ya mbingu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa ilitupasa tuwe na Kuhani Mkuu wa namna hii, yaani aliye mtakatifu, asiye na lawama, asiye na dosari, aliyetengwa na wenye dhambi na kuinuliwa juu ya mbingu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana ilitupasa sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii aliye mtakatifu, asiyekuwa na uovu, asiyekuwa na waa lo lote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo Yesu ni aina ya kuhani mkuu tunayemhitaji. Yeye ni mkamilifu. Hana dhambi ndani yake. Hana kasoro na havutwi na watenda dhambi. Naye amepandishwa juu ya mbingu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, Yesu ndiye Kuhani Mkuu ambaye anatufaa sana katika mahitaji yetu. Yeye ni mtakatifu, hana hatia wala dhambi ndani yake; hayumo katika kundi la wenye dhambi na ameinuliwa mpaka juu mbinguni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, ilikuwa jambo la kufaa sana kwetu kuwa na kuhani kama huyo, mtakatifu, asiye na hatia wala dhambi ndani yake; ametenganishwa mbali na wenye dhambi, na ameinuliwa juu ya mbingu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa ilitupasa tuwe na Kuhani Mkuu wa namna hii, yaani, aliye mtakatifu, asiye na lawama, asiye na dosari, aliyetengwa na wenye dhambi na kuinuliwa juu ya mbingu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa ilitupasa tuwe na Kuhani Mkuu wa namna hii, yaani, aliye mtakatifu, asiye na lawama, asiye na dosari, aliyetengwa na wenye dhambi na kuinuliwa juu ya mbingu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana ilitupasa sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii aliye mtakatifu, asiyekuwa na uovu, asiyekuwa na waa lolote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, ilikuwa jambo la kufaa sana kwetu kuwa na kuhani kama huyo, mtakatifu, asiye na hatia wala dhambi ndani yake; ametenganishwa mbali na wenye dhambi, na ameinuliwa juu ya mbingu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani mtambikaji mkuu, ambaye tunapaswa naye, ni yule mcha Mungu, asiye mwovu, asiye mwenye madoa, aliyetengeka na wakosaji, alioko juu kuliko mbingu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana ilitupasa sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii aliye mtakatifu, asiyekuwa na uovu, asiyekuwa na waa lo lote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi Yesu ndiye Kuhani Mukubwa anayefaa kwa ajili yetu. Yeye ni mutakatifu, hana kosa wala alama ya uchafu. Ametengwa mbali na wenye zambi, naye amenyanyuliwa juu sana mbinguni.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana ilipendeza sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii, aliye mtakatifu, asiokuwa na uovu, asiokuua na waa lolote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu;