Hebrews 7:28 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sheria huwateua watu walio dhaifu kuwa makuhani wakuu; lakini ahadi ya Mungu aliyoifanya kwa kiapo na ambayo imefika baada ya sheria imemteua Mwana ambaye amefanywa mkamilifu milele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa sheria huwaweka makuhani wakuu watu ambao ni dhaifu; lakini lile neno la kiapo, lililokuja baada ya sheria, lilimweka Mwana, ambaye amefanywa kuwa mkamilifu milele.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana torati yawaweka wanadamu walio na unyonge kuwa makuhani wakuu; bali hilo neno la kiapo kilichokuja baada ya torati limemweka Mwana, aliyekamilika hata milele.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sheria huchagua makuhani wakuu ambao ni watu na wanao udhaifu ule ule ambao watu wote wanao. Lakini baada ya sheria, Mungu alisema kiapo ambacho kilimfanya Mwana awe kuhani mkuu. Na Mwana huyo, aliyekamilishwa kwa njia ya mateso, atatumika kama kuhani mkuu milele yote.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Sheria ya Mose huwateua watu waliokuwa dhaifu kuwa makuhani wakuu; lakini ahadi ya Mungu aliyoifanya kwa kiapo na ambayo imefika baada ya sheria imemteua Mwana ambaye amefanywa mkamilifu milele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sheria huwateua watu walio dhaifu kuwa makuhani wakuu; lakini ahadi ya Mungu aliyoifanya kwa kiapo na ambayo imefika baada ya sheria imemteua Mwana ambaye amefanywa mkamilifu milele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa sheria huwaweka makuhani wakuu watu ambao ni dhaifu, lakini lile neno la kiapo, lililokuja baada ya sheria, lilimweka Mwana, ambaye amefanywa kuwa mkamilifu milele.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa sheria huwaweka makuhani wakuu watu ambao ni dhaifu; lakini lile neno la kiapo, lililokuja baada ya sheria, lilimweka Mwana, ambaye amefanywa kuwa mkamilifu milele.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana torati yawaweka wanadamu walio na unyonge kuwa makuhani wakuu; bali hilo neno la kiapo kilichokuja baada ya torati limemweka Mwana, aliyekamilika hata milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sheria huwateua watu walio dhaifu kuwa makuhani wakuu; lakini ahadi ya Mungu aliyoifanya kwa kiapo na ambayo imefika baada ya sheria imemteua Mwana ambaye amefanywa mkamilifu milele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani Maonyo huweka watu wenye unyonge kuwa watambikaji wakuu. Lakini neno la kiapo kilichoyafuata Maonyo nyuma linamweka Mwana kuwa mtambikaji mtimilifu wa kale na kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana torati yawaweka wanadamu walio na unyonge kuwa makuhani wakuu; bali hilo neno la kiapo kilichokuja baada ya torati limemweka Mwana, aliyekamilika hata milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sheria ya Musa inawaweka watu wenye uzaifu kuwa Makuhani Wakubwa, lakini kufuatana na kiapo kilichokuja nyuma ya Sheria ile, Mwana anayekuwa mukamilifu kwa milele aliwekwa kuwa Kuhani Mukubwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana torati yawaweka wana Adamu walio na unyonge kuwa makuhani wakuu; bali neno la kiapo kilichokuja baada ya torati limemweka Mwana, aliyekamilika hatta milele.