Hebrews 7:3 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baba yake na mama yake hawatajwi, wala ukoo wake hautajwi; haisemwi alizaliwa lini au alikufa lini. Anafanana na Mwana wa Mungu, na anaendelea kuwa kuhani daima.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hana baba wala mama, hana ukoo, hana mwanzo wala mwisho wa siku zake, kama Mwana wa Mungu. Yeye adumu akiwa kuhani milele.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hakuna ajuaye baba na mama yake walikuwa ni kina nani au walitokea wapi. Na hakuna ajuaye alizaliwa lini au alikufa lini. Melkizedeki ni kama Mwana wa Mungu kwa vile siku zote atakuwa kuhani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baba yake na mama yake hawatajwi, wala ukoo wake hautajwi; haisemwi alizaliwa lini au alikufa lini. Anafanana na Mwana wa Mungu, na anaendelea kuwa kuhani daima.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baba yake na mama yake hawatajwi, wala ukoo wake hautajwi; haisemwi alizaliwa lini au alikufa lini. Anafanana na Mwana wa Mungu, na anaendelea kuwa kuhani daima.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hana Baba wala mama, hana ukoo, hana mwanzo wala mwisho wa siku zake, kama Mwana wa Mungu, yeye adumu kuhani milele.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hana baba wala mama, hana ukoo, hana mwanzo wala mwisho wa siku zake, kama Mwana wa Mungu. Yeye adumu akiwa kuhani milele.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baba yake na mama yake hawatajwi, wala ukoo wake hautajwi; haisemwi alizaliwa lini au alikufa lini. Anafanana na Mwana wa Mungu, na anaendelea kuwa kuhani daima.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Baba yake na mama yake nao wakale wake hawajuliki, wala siku zake za kuishi hazijuliki, zilipoanzia, wala zilipokomea, maana amefananishwa na Mwana wa Mungu, ni mtambikaji wa kale na kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hakuna mambo yaliyoandikwa juu ya baba ya Melkisedeki, wala mama yake, wala majina ya babu zake. Tena, habari za kuzaliwa kwake na za kufa kwake hazijulikani. Anafanana na Mwana wa Mungu kwa kuwa yeye ni kuhani kwa milele.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhayi wake, bali amefanauishwa na Mwaua wa Mungu,) adumu kuhani milele.