Hebrews 7:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tunajua pia kwamba kufuatana na sheria, wazawa wa Lawi ambao ni makuhani, wanayo haki ya kuchukua sehemu moja ya kumi kutoka kwa watu, yaani ndugu zao, ingawaje nao ni wazawa wa Abrahamu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi sheria inawaagiza wana wa Lawi ambao hufanyika makuhani kupokea sehemu ya kumi kutoka kwa watu ambao ni ndugu zao, ingawa ndugu zao ni wazao wa Ibrahimu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na katika wana wa Lawi nao, wale waupatao ukuhani, wana amri kutwaa sehemu ya kumi kwa watu wao, yaani, ndugu zao, kwa agizo la sheria, ijapokuwa wametoka katika viuno vya Ibrahimu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sasa sheria inasema kwamba wale wa ukoo wa Lawi waliokuja kuwa makuhani wanastahili kupata sehemu ya kumi kutoka kwa watu wao, hata kama wao na watu wao ni wa familia ya Ibrahimu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Tunajua vilevile kwamba kufuatana na Sheria, wana wa Lawi ambao ni makuhani, wanayo haki ya kuchukua sehemu ya kumi kutoka kwa watu, yaani ndugu zao, ingawaje nao ni watoto wa Abrahamu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tunajua pia kwamba kufuatana na sheria, wazawa wa Lawi ambao ni makuhani, wanayo haki ya kuchukua sehemu moja ya kumi kutoka kwa watu, yaani ndugu zao, ingawaje nao ni wazawa wa Abrahamu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi sheria inawaagiza wana wa Lawi wale ambao hufanyika makuhani hupokea sehemu ya kumi kutoka watu, ambao ni ndugu zao, ingawa wao ni wazao wa Abrahamu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi sheria inawaagiza wana wa Lawi ambao hufanyika makuhani kupokea sehemu ya kumi kutoka kwa watu ambao ni ndugu zao, ingawa ndugu zao ni wazao wa Ibrahimu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na katika wana wa Lawi nao, wale waupatao ukuhani, wana amri kutwaa sehemu ya kumi kwa watu wao, yaani, ndugu zao, kwa agizo la sheria, ijapokuwa wametoka katika uzao wa Abrahamu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tunajua pia kwamba kufuatana na sheria, wazawa wa Lawi ambao ni makuhani, wanayo haki ya kuchukua sehemu moja ya kumi kutoka kwa watu, yaani ndugu zao, ingawaje nao ni wazawa wa Abrahamu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kweli nao wana wa Lawi waliopewa utambikaji waliagizwa na Maonyo kuwatoza fungu la kumi wenzao wa ukoo walio ndugu zao, tena ndio waliotoka pamoja nao kiunoni mwa Aburahamu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na katika wana wa Lawi nao, wale waupatao ukuhani, wana amri kutwaa sehemu ya kumi kwa watu wao, yaani, ndugu zao, kwa agizo la sheria, ijapokuwa wametoka katika viuno vya Ibrahimu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wazao wa Lawi wanaopewa kazi ya ukuhani wanaamriwa na Sheria kukongoa fungu moja la kumi la mapato toka kwa wandugu zao Waisraeli, ijapokuwa wao vilevile ni wa uzao wa Abrahamu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na katika wana wa Lawi, wale waupatao ukuhani, wana amri kutwaa sehemu ya kumi kwa watu wao, yaani ndugu zao, kwa agizo la sharia, ijapokuwa wametoka katika viuno vya Ibrahimu.