Hebrews 7:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena, hao makuhani wanaopokea sehemu ya kumi, ni watu ambao hufa; lakini hapa anayepokea sehemu ya kumi, yaani Melkisedeki, anasemekana kwamba hafi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa upande mmoja, sehemu ya kumi hupokelewa na watu ambao hufa; lakini kwa upande mwingine hupokelewa na yeye ambaye hushuhudiwa kuwa yu hai.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na hapa wanadamu wapatikanao na kufa hutwaa sehemu ya kumi; bali huko yeye ashuhudiwaye kwamba yu hai.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Makuhani hawa hupata sehemu ya kumi, lakini wao ni binadamu tu wanaoishi kisha hufa. Lakini Melkizedeki, aliyepata sehemu ya kumi kutoka kwa Ibrahimu, anaendelea kuishi, kama Maandiko yanavyosema.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Tena, hao makuhani wanaopokea sehemu ya kumi, ni watu ambao hufa; lakini hapa anayepokea sehemu ya kumi, yaani Melkisedeki, anasemekana kwamba hafi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena, hao makuhani wanaopokea sehemu ya kumi, ni watu ambao hufa; lakini hapa anayepokea sehemu ya kumi, yaani Melkisedeki, anasemekana kwamba hafi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa upande mmoja, sehemu ya kumi hupokelewa na wale ambao hupatikana na kufa; lakini kwa upande mwingine hupokelewa na yeye ambaye hushuhudiwa kuwa yu hai.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa upande mmoja, sehemu ya kumi hupokelewa na wale ambao hupatikana na kufa; lakini kwa upande mwingine hupokelewa na yeye ambaye hushuhudiwa kuwa yu hai.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na hapa wanadamu wapatikanao na kufa hutwaa sehemu ya kumi; bali huko yeye ashuhudiwaye kwamba yuko hai.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena, hao makuhani wanaopokea sehemu ya kumi, ni watu ambao hufa; lakini hapa anayepokea sehemu ya kumi, yaani Melkisedeki, anasemekana kwamba hafi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Napo hapo watu walio wenye kufa hutoza fungu la kumi; lakini alilitoza mtu anayeshuhudiwa kwamba: Anaishi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na hapa wanadamu wapatikanao na kufa hutwaa sehemu ya kumi; bali huko yeye ashuhudiwaye kwamba yu hai.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale makuhani wanaopokea fungu la kumi ni watu wanaokufa; lakini Melkisedeki aliyepokea fungu la kumi anashuhudiwa kwamba anaishi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na hapo wana Adamu wapaswao na kufa hutwaa sehemu ya kumi; bali huku yeye ashubudiwae kwamba yu hayi.