Hebrews 8:1 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, jambo muhimu katika hayo tunayosema ni hili: Sisi tunaye kuhani mkuu wa namna hiyo, ambaye anaketi upande wa kulia wa kiti cha enzi cha Mkuu mbinguni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi jambo tunalotaka kulisema ni hili: Tunaye Kuhani Mkuu aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Aliye Mkuu mbinguni,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hii ndiyo hoja tunayosema: Tunaye kuhani mkuu wa jinsi hiyo, anayeketi upande wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu Mkuu mbinguni.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, jambo muhimu katika hayo tunayosema ni hili: sisi tunaye Kuhani Mkuu wa namna hiyo, ambaye anaketi upande wa kulia wa kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu mbinguni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, jambo muhimu katika hayo tunayosema ni hili: sisi tunaye kuhani mkuu wa namna hiyo, ambaye anaketi upande wa kulia wa kiti cha enzi cha Mkuu mbinguni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi jambo tunalotaka kulisema ni hili: Tunaye Kuhani Mkuu ambaye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi jambo tunalotaka kulisema ni hili: Tunaye Kuhani Mkuu ambaye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Aliye Mkuu mbinguni,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, jambo muhimu katika hayo tunayosema ni hili: Sisi tunaye kuhani mkuu wa namna hiyo, ambaye anaketi upande wa kulia wa kiti cha enzi cha Mkuu mbinguni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Neno lililo kuu katika hayo, tuliyoyasema, ni hili: Tunaye mtambikaji mkuu aliyeketi mbinguni kuumeni kwa kiti cha kifalme chenye ukuu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Jambo la lazima sana katika maneno tunayosema sasa ni hili. Tuko na Mukubwa wa namna ile, anayeikaa na mamlaka katika mbingu kwa kuume kwa Mwenyezi Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
BASSI, katika hayo tuuayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunae kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha ukuu mbinguni,