Hebrews 8:10 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hili ndilo agano nitakalofanya na watu wa Israeli siku zijazo, asema Bwana: Nitaweka sheria zangu akilini mwao, na kuziandika mioyoni mwao. Mimi nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hili ndilo agano nitakalofanya na nyumba ya Israeli baada ya siku zile, asema Mwenyezi Mungu. Nitaziweka sheria zangu katika nia zao na kuziandika mioyoni mwao. Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu wangu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hili ni agano jipya nitakalofanya na watu wa Israeli siku zijazo, asema Bwana: Nitaziweka sheria zangu katika fahamu zao, na nitaandika sheria zangu katika mioyo yao. Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Na hili ndilo agano nitakalofanya na watu wa Israeli siku zijazo, asema Bwana: Nitaweka sheria zangu akilini mwao, na kuziandika mioyoni mwao. Mimi nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hili ndilo agano nitakalofanya na watu wa Israeli siku zijazo, asema Bwana: Nitaweka sheria zangu akilini mwao, na kuziandika mioyoni mwao. Mimi nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya siku zile, hili ndilo Agano nitakalofanya na nyumba ya Israeli, asema Bwana. Nitaweka sheria zangu katika nia zao na kuziandika katika mioyo yao. Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hili ndilo agano nitakalofanya na nyumba ya Israeli baada ya siku zile, asema Mwenyezi Mungu. Nitaziweka sheria zangu katika nia zao na kuziandika mioyoni mwao. Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika fikira zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu wangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hili ndilo agano nitakalofanya na watu wa Israeli siku zijazo, asema Bwana: Nitaweka sheria zangu akilini mwao, na kuziandika mioyoni mwao. Mimi nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani Bwana asema: Agano, nitakalolifanya nao wa mlango wa Isiraeli, siku hizi zitakapokuwa zimepita, ni hili, asema Bwana: Nitawapa Maonyo yangu, yakae katika mawazo yao, tena nitayaandika mioyoni mwao; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu wangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa hili ndilo agano nitakalofanya na watu wa ufalme wa Israeli katika siku zile: nitawawezesha kuchunga sheria zangu ndani ya mafikiri yao, nikiziandika ndani ya mioyo yao. Ni Bwana wetu Mungu anayesema hivyo. Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana hili ndilo agano nitakalofanyana na nyumba ya Israeli baada ya siku zile, asema Bwana; nitatia sharia zangu katika nia zao, na katika mioyo yao nitaziandika; nami mtakuwa Mungu kwao, nao watakuwa watu waugu.