Hebrews 8:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hakuna atakayemfundisha mwananchi mwenzake, wala atakayemwambia ndugu yake: ‘Mjue Bwana’. Maana wote, wadogo na wakubwa, watanijua mimi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtu hatamfundisha tena jirani yake, wala mtu kumfundisha ndugu yake akisema, ‘Mjue Mwenyezi Mungu,’ kwa sababu wote watanijua mimi, tangu aliye mdogo kabisa kwao, hadi aliye mkuu sana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao hawatafundishana kila mtu na jirani yake, Na kila mtu na ndugu yake, akisema, Mjue Bwana; Kwa maana wote watanijua, Tangu mdogo wao hata mkubwa wao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hakuna tena atakayemfundisha jirani yake au familia yake kumjua Bwana. Watu wote, wakuu zaidi na wasio na umuhimu kabisa, watanijua.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hakuna mtu atakayemfundisha mwananchi mwenzake, wala atakayemwambia ndugu yake: Mjue Bwana. Maana watu wote, wadogo na wakubwa, watanijua mimi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hakuna atakayemfundisha mwananchi mwenzake, wala atakayemwambia ndugu yake: ‘Mjue Bwana’. Maana wote, wadogo na wakubwa, watanijua mimi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtu hatamfundisha tena jirani yake, wala mtu hatamfundisha ndugu yake akisema, ‘Mjue Bwana,’ kwa sababu wote watanijua mimi, tangu aliye mdogo wa wote hadi aliye mkuu sana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtu hatamfundisha tena jirani yake, wala mtu kumfundisha ndugu yake akisema, ‘Mjue Bwana Mwenyezi,’ kwa sababu wote watanijua mimi, tangu aliye mdogo kabisa kwao, hadi aliye mkuu sana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao hawatafundishana kila mtu na jirani yake, Na kila mtu na ndugu yake, akisema, Mjue Bwana; Kwa maana wote watanijua, Tangu mdogo wao hata mkubwa wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hakuna atakayemfundisha mwananchi mwenzake, wala atakayemwambia ndugu yake: ‘Mjue Bwana’. Maana wote, wadogo na wakubwa, watanijua mimi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hawatafundishana tena mtu na mwenziwe wala mtu na ndugu yake kwamba: Mtambue Bwana! Kwani wote watanijua, hivyo walivyo wadogo, mpaka wakiwa wakubwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao hawatafundishana kila mtu na jirani yake, Na kila mtu na ndugu yake, akisema, Mjue Bwana; Kwa maana wote watanijua, Tangu mdogo wao hata mkubwa wao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hakutakuwa tena atakayefundisha mwanainchi mwenzake, au kumwambia ndugu yake: ‘Umujue Bwana.’ Kwa maana watu wote watanijua, tangu mudogo mpaka mukubwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nao hawatafundishana killa mtu na jirani yake, na killa mtu na ndugu yake, akisema, Mjue Bwana; kwa maana wote watunijua, tangu mdogo wao hatta mkubwa wao.