Hebrews 8:13 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa kusema juu ya agano jipya, Mungu alilichakaza lile la kwanza; na chochote kinachochakaa na kuwa kikuukuu kitatoweka karibuni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuliita agano hili “jipya”, Mungu amefanya lile agano la kwanza kuwa kuukuu; nacho kitu kinachoanza kuchakaa na kuwa kikuukuu kiko karibu kutoweka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mungu aliliita hili ni agano jipya, hivyo amelifanya agano la kwanza kuwa la zamani. Na chochote kilicho cha zamani na kisichokuwa na matumizi kiko tayari kutoweka.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa kusema juu ya agano jipya, Mungu alilichakaza lile la kwanza; na chochote kinachochakaa na kuwa kikuukuu kitatoweka karibuni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa kusema juu ya agano jipya, Mungu alilichakaza lile la kwanza; na chochote kinachochakaa na kuwa kikuukuu kitatoweka karibuni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuliita Agano hili “jipya” Mungu amefanya lile Agano la kwanza kuwa kuukuu; nacho kitu kinachoanza kuchakaa na kuwa kikuukuu kiko karibu kutoweka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuliita agano hili “jipya,” Mwenyezi Mungu amefanya lile agano la kwanza kuwa kuukuu; nacho kitu kinachoanza kuchakaa na kuwa kikuukuu kiko karibu kutoweka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa kiko karibu kutoweka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa kusema juu ya agano jipya, Mungu alilichakaza lile la kwanza; na chochote kinachochakaa na kuwa kikuukuu kitatoweka karibuni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Agano anapoliita Jipya, lile la kwanza amekwisha kulifanya kukuu. Lakini lililo kukuu na chakavu limefikia kutoweka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu alipotangaza hilo agano kuwa “jipya”, jambo hilo lilisababisha lile la kwanza kuwa la zamani na lenye kuchakaa. Na kitu chochote kikiwa cha zamani na chenye kuchakaa kinafikia wakati wa kutoweka.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikukuu na kuchakaa ni karibu na kutoweka.