Hebrews 8:3 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila kuhani mkuu ameteuliwa kumtolea Mungu zawadi na tambiko, na hivyo kuhani mkuu wetu lazima naye awe na kitu cha kutolea.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kila kuhani mkuu huwekwa ili atoe sadaka na dhabihu. Vivyo hivyo, ilikuwa jambo muhimu kwa huyu Kuhani naye awe na kitu cha kutoa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana kila kuhani mkuu huwekwa ili atoe vipawa na dhabihu; kwa hiyo lazima huyu naye awe na kitu cha kutoa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kila kuhani mkuu anayo kazi ya kutoa sadaka na sadaka kwa Mungu. Hivyo kuhani wetu mkuu pia anahitajika kutoa kitu kwa Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kila Kuhani Mkuu ameteuliwa kumtolea Mungu vipawa na dhabihu, na hivyo Kuhani Mkuu wetu lazima pia awe na kitu cha kutolea.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila kuhani mkuu ameteuliwa kumtolea Mungu zawadi na tambiko, na hivyo kuhani mkuu wetu lazima naye awe na kitu cha kutolea.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kila Kuhani Mkuu huwekwa ili atoe sadaka na dhabihu. Vivyo hivyo ilikuwa jambo muhimu kwa huyu Kuhani naye awe na kitu cha kutoa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kila kuhani mkuu huwekwa ili atoe sadaka na dhabihu. Vivyo hivyo, ilikuwa jambo muhimu kwa huyu Kuhani naye awe na kitu cha kutoa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana kila kuhani mkuu huwekwa ili atoe vipawa na dhabihu; kwa hiyo lazima huyu naye awe na kitu cha kutoa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila kuhani mkuu ameteuliwa kumtolea Mungu zawadi na tambiko, na hivyo kuhani mkuu wetu lazima naye awe na kitu cha kutolea.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani kila mtambikaji huwekwa kupeleka matoleo na vipaji vya tambiko. Kwa hiyo hata huyu amepaswa kuwa na kitu cha kumpelekea Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana kila kuhani mkuu huwekwa ili atoe vipawa na dhabihu; kwa hiyo lazima huyu naye awe na kitu cha kutoa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila Kuhani Mukubwa anawekwa kusudi afanye kazi ya kutoa sadaka na matoleo. Kufuatana na hiyo, ilimupasa Kuhani wetu Mukubwa Kristo akuwe na kitu cha kutoa vilevile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana killa kuhani mkuu awekwa illi atoe vipawa na dhabihu; kwa hiyo lazima huyu nae awe na kitu akitoe.