Hebrews 8:5 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huduma zao za kikuhani ni mfano tu na kivuli cha yale yaliyoko mbinguni. Maana Mose alipokuwa karibu kuitengeneza ile maskani, Mungu alimwambia: “Tengeneza kila kitu kufuatana na ule mfano uliooneshwa kule mlimani.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wanahudumu katika patakatifu palipo mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni. Hii ndiyo sababu Musa alionywa alipokaribia kujenga Maskani, akaambiwa: “Hakikisha kuwa unavitengeneza vitu vyote kwa mfano uliooneshwa kule mlimani.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
watumikiao mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile hema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kazi ambayo makuhani hawa wanafanya hakika ni nakala tu na kivuli cha yaliyoko mbinguni. Ndiyo sababu Mungu alimwonya Musa alipokuwa amejiandaa kujenga Hema Takatifu: “Uwe na uhakika kufanya kila kitu sawasawa na kielelezo nilichokuonesha kule mlimani.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Huduma zao za kikuhani ni mfano tu na kivuli cha yale yaliyoko mbinguni. Ndivyo pia ilivyokuwa kwa Mose. Wakati alipokuwa karibu kuitengeneza ile hema, Mungu alimwambia: “Tengeneza kila kitu kufuatana na ule mfano ulioonyeshwa kule mlimani.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huduma zao za kikuhani ni mfano tu na kivuli cha yale yaliyoko mbinguni. Maana Mose alipokuwa karibu kuitengeneza ile maskani, Mungu alimwambia: “Tengeneza kila kitu kufuatana na ule mfano uliooneshwa kule mlimani.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wanahudumu katika patakatifu palipo mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni. Hii ndiyo sababu Mose alionywa alipokaribia kujenga hema, akiambiwa: “Hakikisha kuwa unafanya kila kitu sawasawa na kile kielelezo ulichoonyeshwa kule mlimani.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wanahudumu katika patakatifu palipo mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni. Hii ndiyo sababu Musa alionywa alipokaribia kujenga hema, akiambiwa: “Hakikisha kuwa unavitengeneza vitu vyote kwa mfano ulioonyeshwa kule mlimani.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
watumikiao mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile hema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule uliooneshwa katika mlima.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huduma zao za kikuhani ni mfano tu na kivuli cha yale yaliyoko mbinguni. Maana Mose alipokuwa karibu kuitengeneza ile maskani, Mungu alimwambia: “Tengeneza kila kitu kufuatana na ule mfano uliooneshwa kule mlimani.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao huvitumikia vile vilivyo mfano na kivuli cha vile vilivyoko mbinguni. Ndivyo, Mose naye alivyoagizwa alipotaka kulitengeneza lile hema, kwamba: Angalia, uyafanye yote kwa mfano, ulioonyeshwa mlimani!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
watumikiao mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile hema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kazi wale makuhani wanayofanya ni mufano na kitambulisho kinachoonyesha jinsi mambo kamili yanavyopitika mbinguni. Maneno hayo yanalingana na yale yaliyomutokea Musa. Wakati Musa alipokuwa karibu ya kujenga Hema, Mungu alimwambia: “Ufanye angalisho kusudi upate kutengeneza kila kitu kufuatana na mufano niliokuonyesha kwa mulima.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
watumikao kwa mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile khema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima.