Hebrews 8:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini sasa Yesu amepewa huduma ya kikuhani iliyo bora kuliko yao, kama vile agano alilothibitisha kati ya watu na Mungu ni bora zaidi, kwani lina msingi wake katika ahadi za mambo yaliyo bora zaidi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini huduma aliyopewa Isa ni bora kuliko yao, kama vile agano ambalo yeye ni mpatanishi wake lilivyo bora zaidi ya lile la zamani, nalo limewekwa misingi ya ahadi zilizo bora zaidi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini sasa amepata huduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe wa agano lililo bora, lililoamriwa juu ya ahadi zilizo bora.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini kazi ambayo tayari imetolewa kwa Yesu ni kuu zaidi ya kazi iliyotolewa na makuhani hao. Kwa jinsi hiyo hiyo, agano jipya ambalo Yesu alilileta kutoka kwa Mungu kuja kwa watu wake ni kuu zaidi kuliko lile la zamani. Na agano jipya limeelemea katika ahadi bora zaidi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini sasa Yesu amepewa huduma ya kikuhani iliyo bora zaidi kuliko yao, kama vile agano alilothibitisha kati ya watu na Mungu ni bora zaidi, kwani lina msingi wake katika ahadi za mambo yaliyo bora zaidi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini sasa Yesu amepewa huduma ya kikuhani iliyo bora kuliko yao, kama vile agano alilothibitisha kati ya watu na Mungu ni bora zaidi, kwani lina msingi wake katika ahadi za mambo yaliyo bora zaidi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini huduma aliyopewa Yesu ni bora zaidi kuliko yao kama vile lile Agano ambalo yeye ni mjumbe wake lilivyo bora zaidi kuliko lile la zamani, nalo limewekewa misingi juu ya ahadi zilizo bora zaidi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini huduma aliyopewa Isa ni bora zaidi kuliko yao, kama vile agano ambalo yeye ni mpatanishi wake lilivyo bora zaidi kuliko lile la zamani, nalo limewekwa misingi wa ahadi zilizo bora zaidi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini sasa amepata huduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe wa agano lililo bora, lililoamriwa juu ya ahadi zilizo bora.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini sasa Yesu amepewa huduma ya kikuhani iliyo bora kuliko yao, kama vile agano alilothibitisha kati ya watu na Mungu ni bora zaidi, kwani lina msingi wake katika ahadi za mambo yaliyo bora zaidi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini sasa huyu amepata utumikizi ulioupita, kwani agano, alilotuletea, ni zuri kuliko lile, tena limeunganishwa na maagizo na viagio vilivyo vizuri navyo kuliko vile.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini sasa amepata huduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe wa agano lililo bora, lililoamriwa juu ya ahadi zilizo bora.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini sasa Yesu amepewa kazi inayokuwa bora zaidi kuliko kazi ya wale makuhani, kwa maana yeye ni mupatanishi wa agano linalokuwa zuri zaidi. Sherti za agano lile zinasimamia juu ya ahadi ya Mungu inayokuwa bora zaidi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini sasa amepata khuduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mtengenezaji wa agano lililo bora, lililoamriwa kwa ahadi zilizo bora na kuzitegemea.