Hebrews 8:9 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Agano hili halitakuwa kama lile nililofanya na babu zao siku nilipowaongoza kwa mkono kutoka Misri. Hawakuwa waaminifu kwa agano langu; na hivyo mimi sikuwajali, asema Bwana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Agano langu halitakuwa kama lile nililofanya na baba zao nilipowashika mkono kuwaongoza watoke nchi ya Misri, kwa sababu hawakuendelea kuwa waaminifu katika agano langu, nami nikawaacha, asema Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Halitakuwa kama agano lile nililoagana na baba zao, Katika siku ile nilipowashika mikono yao niwatoe katika nchi ya Misri. Kwa sababu hawakudumu katika agano langu, Mimi nami sikuwajali asema Bwana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Halitakuwa sawa na agano lililotengenezwa na baba zao. Hilo ni agano nililowapa nilipowachukua kwa mkono na kuwatoa Misri. Hawakuendelea kufuata agano nililowekeana nao, na nikageuka mbali nao, asema Bwana.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Agano hili halitakuwa kama lile nililofanya na babu zao siku ile nilipowaongoza kwa mkono kutoka nchi ya Misri. Hawakuwa waaminifu kwa agano langu; na hivyo mimi sikuwajali, asema Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Agano hili halitakuwa kama lile nililofanya na babu zao siku nilipowaongoza kwa mkono kutoka Misri. Hawakuwa waaminifu kwa agano langu; na hivyo mimi sikuwajali, asema Bwana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Agano langu halitakuwa kama lile nililofanya na baba zao nilipowashika mkono ili kuwatoa katika nchi ya Misri, kwa kuwa hawakuendelea kuwa waaminifu katika Agano langu, nami nikawaacha, asema Bwana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Agano langu halitakuwa kama lile nililofanya na baba zao nilipowashika mkono kuwaongoza watoke nchi ya Misri, kwa sababu hawakuendelea kuwa waaminifu katika agano langu, nami nikawaacha, asema Bwana Mwenyezi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Halitakuwa kama agano lile nililoagana na baba zao, Katika siku ile nilipowashika mikono yao niwatoe katika nchi ya Misri. Kwa sababu hawakudumu katika agano langu, Mimi nami sikuwajali asema Bwana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Agano hili halitakuwa kama lile nililofanya na babu zao siku nilipowaongoza kwa mkono kutoka Misri. Hawakuwa waaminifu kwa agano langu; na hivyo mimi sikuwajali, asema Bwana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Halitakuwa, kama Agano lile lilivyokuwa, nililolifanya na baba zao siku ile, nilipowashika mikono, niwatoe katika nchi ya Misri; kwani wao wenyewe hawakulishika Agano langu, nami nikawakataa; ndivyo, asemavyo Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Halitakuwa kama agano lile nililoagana na baba zao, Katika siku ile nilipowashika mikono yao niwatoe katika nchi ya Misri. Kwa sababu hawakudumu katika agano langu, Mimi nami sikuwajali asema Bwana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Agano lile halitakuwa sawa na lile nililofanya na babu zao siku nilipowakamatia kwenye mukono na kuwaondoa toka inchi ya Misri. Kwa sababu hawakushika lile agano, kwa hiyo vilevile sikuwashugulikia. Ni Bwana wetu Mungu anayesema hivyo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa sababu hawakudumu katika agano langu, mimi nami sikuwaangalia, asema Bwana.