Hebrews 9:15 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo yeye ni mpatanishi wa agano jipya ambamo wale walioitwa na Mungu wanaweza kupokea baraka za milele walizoahidiwa. Kifo chake huwakomboa watu kutoka yale makosa waliyofanya wakati wa lile agano la kale.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa sababu hii Al-Masihi ni mpatanishi wa agano jipya, ili wale walioitwa waweze kupokea ile ahadi ya urithi wa milele: kwa vile yeye alikufa awe ukombozi wao kutoka kwa dhambi walizozitenda chini ya agano la kwanza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kwa sababu hii ni mjumbe wa agano jipya, ili, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa yaliyokuwa chini ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee ahadi ya urithi wa milele.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo Kristo huwaletea watu wake agano jipya kutoka kwa Mungu. Huleta agano hili ili wale walioteuliwa na Mungu waweze kuzipata baraka ambazo Mungu aliwaahidi, baraka zinazodumu milele. Hili laweza kutokea tu kwa sababu Kristo alikufa ili awaweke huru watu kutokana na dhambi zilizotendwa dhidi ya amri za agano la kwanza.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa hiyo, Kristo ndiye aliyeratibisha agano jipya ili wale walioitwa na Mungu wazipokee baraka za milele walizoahidiwa. Watazipata, kwani kifo kimetokea ambacho huwakomboa watu kutoka yale makosa waliyofanya wakati wa lile agano la kale.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo yeye ni mpatanishi wa agano jipya ambamo wale walioitwa na Mungu wanaweza kupokea baraka za milele walizoahidiwa. Kifo chake huwakomboa watu kutoka yale makosa waliyofanya wakati wa lile agano la kale.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa sababu hii Kristo ni mjumbe wa Agano Jipya, ili kwamba wale walioitwa waweze kupokea ile ahadi ya urithi wa milele, yeye alikufa awe ukombozi wao kutoka katika dhambi walizozitenda chini ya Agano la kwanza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa sababu hii Al-Masihi ni mpatanishi wa agano jipya, ili kwamba wale walioitwa waweze kupokea ile ahadi ya urithi wa milele: kwa vile yeye alikufa awe ukombozi wao kutoka kwa dhambi walizozitenda chini ya agano la kwanza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kwa sababu hii ni mjumbe wa agano jipya, ili, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa yaliyokuwa chini ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee ahadi ya urithi wa milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo yeye ni mpatanishi wa agano jipya ambamo wale walioitwa na Mungu wanaweza kupokea baraka za milele walizoahidiwa. Kifo chake huwakomboa watu kutoka yale makosa waliyofanya wakati wa lile agano la kale.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa sababu hii alikuwa mpatanishi aliyetuletea Agano Jipya kwamba: Walioitwa na waupate urithi wao ulio wa kale na kale, kama walivyoagiwa, kwani kufa kumeoneka kunakokomboa katika makosa yaliyofanyika siku za Agano la kwanza.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kwa sababu hii ni mjumbe wa agano jipya, ili, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa yaliyokuwa chini ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee ahadi ya urithi wa milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa sababu hii, Kristo ni mupatanishi wa agano jipya. Kwa njia ya kufa kwake aliwakomboa watu toka katika makosa waliyofanya chini ya uongozi wa agano la kwanza, kusudi wale walioalikwa na Mungu wapate kupokea urizi wa milele aliowaahidia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na kwa sababu hii yu mjumbe wa agauo jipya, illi, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa ya katika agano la kwanza, walioitiwa waipokee ahadi ya urithi wa milele.