Hebrews 9:19 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwanza Mose aliwatangazia watu wote amri zote kama ilivyokuwa katika sheria; kisha akachukua damu ya ndama pamoja na maji, na kwa majani ya mti wa husopo na pamba nyekundu, akakinyunyizia kile kitabu cha sheria na watu wote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Musa alipotangaza kila amri kwa watu wote, alichukua damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji, sufu nyekundu na matawi ya mti wa hisopo, akanyunyizia kile kitabu na watu wote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana kila amri ilipokwisha kunenwa na Musa kwa hao watu wote, kama ilivyoamuru sheria, aliitwaa damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji na sufu nyekundu na hisopo, akakinyunyizia kitabu chenyewe, na watu wote,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwanza, Musa aliwaeleza watu kila agizo katika sheria. Kisha akachukua damu ya ndama dume na kuichanganya na maji. Alitumia sufu nyekundu na tawi la hisopo kunyunyiza damu na maji katika kitabu cha sheria na kwa watu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwanza Mose aliwatangazia watu wote amri zote kama ilivyokuwa katika Sheria; kisha akachukua damu ya ndama pamoja na maji, na kwa kutumia majani ya mti uitwao husopo na pamba nyekundu, akakinyunyizia kile kitabu cha Sheria na hao watu wote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwanza Mose aliwatangazia watu wote amri zote kama ilivyokuwa katika sheria; kisha akachukua damu ya ndama pamoja na maji, na kwa majani ya mti wa husopo na pamba nyekundu, akakinyunyizia kile kitabu cha sheria na watu wote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati Mose alipotangaza kila amri kwa watu wote, alichukua damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji, sufu nyekundu na matawi ya mti wa hisopo, akanyunyizia kile kitabu na watu wote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Musa alipotangaza kila amri kwa watu wote, alichukua damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji, sufu nyekundu na matawi ya mti wa hisopo, akanyunyizia kile kitabu na watu wote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana kila amri ilipokwisha kunenwa na Musa kwa hao watu wote, kama ilivyoamuru sheria, aliitwaa damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji na sufu nyekundu na hisopo, akakinyunyizia kitabu chenyewe, na watu wote,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwanza Mose aliwatangazia watu wote amri zote kama ilivyokuwa katika sheria; kisha akachukua damu ya ndama pamoja na maji, na kwa majani ya mti wa husopo na pamba nyekundu, akakinyunyizia kile kitabu cha sheria na watu wote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani Mose alipokwisha kuwaambia watu wote kila agizo la maonyo, akachukua damu za ndama na za mbuzi, kisha akachukua na maji na pamba nyekundu na kivumbasi, akakinyunyizia Kitabu chenyewe, kisha nao watu wote,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana kila amri ilipokwisha kunenwa na Musa kwa hao watu wote, kama ilivyoamuru sheria, aliitwaa damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji na sufu nyekundu na hisopo, akakinyunyizia kitabu chenyewe, na watu wote,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana, kwanza Musa aliwatangazia watu wote amri zote za Sheria. Kisha akatwaa damu ya ngombe pamoja na maji, naye akavinyunyiza juu ya kitabu cha Sheria na juu ya watu wote akitumia manyoya mekundu na vitawi vya muti wa hisopo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana killa amri ilipokwisha kunenwa na Musa kwa watu wote, kama ilivyoamuru sharia, aliitwaa damu ya ndama na ya mbuzi pamoja na maji na sufu nyekundu na husopo, akakinyunyizia kitabu chenyewe, na watu wote,