Hebrews 9:2 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Palitengenezwa hema ambayo sehemu yake ya nje iliitwa Mahali Patakatifu. Humo mlikuwa na kinara cha taa, meza na mikate iliyowekwa mbele ya Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hema ilitengenezwa. Katika sehemu yake ya kwanza kulikuwa na kinara cha taa, meza na mikate iliyowekwa wakfu; hii sehemu iliitwa Mahali Patakatifu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana hema ilitengenezwa, ile ya kwanza, mlimokuwa na kinara cha taa, na meza, na mikate ya Wonyesho; ndipo palipoitwa, Patakatifu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mahali hapa palikuwa ni ndani ya hema. Eneo la kwanza ndani ya hema liliitwa Patakatifu. Katika Patakatifu kulikuwepo taa na meza iliyokuwa na mikate maalumu iliyotolewa kwa Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Palitengenezwa hema ambayo sehemu yake ya nje iliitwa Mahali Patakatifu. Humo mlikuwa na kinara cha taa, meza na mikate iliyotolewa kwa Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Palitengenezwa hema ambayo sehemu yake ya nje iliitwa Mahali Patakatifu. Humo mlikuwa na kinara cha taa, meza na mikate iliyowekwa mbele ya Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hema lilitengenezwa, katika sehemu yake ya kwanza kulikuwa na kinara cha taa, meza na mikate iliyowekwa wakfu, hii sehemu iliitwa Mahali Patakatifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hema ilitengenezwa. Katika sehemu yake ya kwanza kulikuwa na kinara cha taa, meza na mikate iliyowekwa wakfu; hii sehemu iliitwa Mahali Patakatifu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana hema ilitengenezwa, ile ya kwanza, mlimokuwa na kinara cha taa, na meza, na mikate mitakatifu; ndipo palipoitwa, Patakatifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Palitengenezwa hema ambayo sehemu yake ya nje iliitwa Mahali Patakatifu. Humo mlikuwa na kinara cha taa, meza na mikate iliyowekwa mbele ya Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani palikuwa pamesimamishwa hema la kuingilia; mwake mlikuwamo taa na meza na mikate aliyowekewa Bwana. Ndipo palipoitwa Patakatifu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana hema ilitengenezwa, ile ya kwanza, mlimokuwa na kinara cha taa, na meza, na mikate ya Wonyesho; ndipo palipoitwa, Patakatifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kufuatana na ile, kulikuwa Hema iliyosimikwa. Chumba chake cha kwanza kiliitwa Pahali Patakatifu. Ndani ya chumba kile kulikuwa kinara cha kuwekea taa, meza na mikate iliyotolewa kwa Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana khema ilitengenezwa, ile ya kwanza, mlimokuwa na taa, na meza, na mikate iliyotolewa kwa Mungu; palipoitwa, Patakatifu.