Hebrews 9:25 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kuhani mkuu wa Wayahudi huingia Mahali Patakatifu kila mwaka akiwa na damu ya mnyama; lakini Kristo hakuingia humo ili ajitoe mwenyewe mara nyingi,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wala hakuingia mbinguni ili apate kujitoa mwenyewe mara kwa mara, kama vile kuhani mkuu aingiavyo Patakatifu pa Patakatifu kila mwaka kwa damu ambayo si yake mwenyewe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wala si kwamba ajitoe mara nyingi, kama vile kuhani mkuu aingiavyo katika patakatifu kila mwaka kwa damu isiyo yake;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kuhani mkuu huingia katika Patakatifu pa Patakatifu mara moja tu kila mwaka. Huchukua pamoja naye damu ya sadaka. Lakini hatoi damu yake kama alivyofanya Kristo. Kristo alienda mbinguni, lakini siyo kujitoa mwenyewe mara nyingi kama ambavyo kuhani mkuu hutoa damu tena na tena.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kuhani Mkuu wa Wayahudi huingia Mahali Patakatifu kila mwaka akiwa amechukua damu ya mnyama; lakini Kristo hakuingia humo ili ajitoe mwenyewe mara nyingi,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kuhani mkuu wa Wayahudi huingia Mahali Patakatifu kila mwaka akiwa na damu ya mnyama; lakini Kristo hakuingia humo ili ajitoe mwenyewe mara nyingi,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wala hakuingia mbinguni ili apate kujitoa mwenyewe mara kwa mara, kama vile Kuhani Mkuu aingiavyo Patakatifu pa Patakatifu kila mwaka kwa damu ambayo si yake mwenyewe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wala hakuingia mbinguni ili apate kujitoa mwenyewe mara kwa mara, kama vile kuhani mkuu aingiavyo Patakatifu pa Patakatifu kila mwaka kwa damu ambayo si yake mwenyewe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wala si kwamba ajitoe mara nyingi, kama vile kuhani mkuu aingiavyo katika patakatifu kila mwaka kwa damu isiyo yake;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kuhani mkuu wa Wayahudi huingia Mahali Patakatifu kila mwaka akiwa na damu ya mnyama; lakini Kristo hakuingia humo ili ajitoe mwenyewe mara nyingi,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini hakuingia, ajitoe mara nyingi, kama mtambikaji mkuu anavyopaingia Patakatifu kila mwaka na kupeleka damu isiyo yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wala si kwamba ajitoe mara nyingi, kama vile kuhani mkuu aingiavyo katika patakatifu kila mwaka kwa damu isiyo yake;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kuhani Mukubwa wa Wayuda anaingia katika Pahali Patakatifu Sana kila mwaka, akibeba damu ya nyama. Lakini Kristo hakuingia humo kusudi ajitoe mwenyewe sadaka mara nyingi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
wala si kusudi ajitoe marra nyiugi, kama vile kuhani mkuu aingiavyo patakatifu killa mwaka kwa damu isiyo yake;