Hebrews 9:4 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Humo mlikuwa na madhabahu ya dhahabu kwa ajili ya kufukizia ubani, na sanduku la agano, ambalo lilikuwa limepakwa dhahabu pande zote, na ndani yake mlikuwa na chungu cha dhahabu kilichokuwa na mana, fimbo ya Aroni iliyokuwa imechanua majani, na vile vibao viwili vya mawe vilivyoandikwa agano.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
ambapo palikuwa na yale madhabahu ya dhahabu ya kufukizia uvumba, na lile Sanduku la Agano lililofunikwa kwa dhahabu. Sanduku hili lilikuwa na gudulia la dhahabu lenye mana, ile fimbo ya Haruni iliyochipuka, na vile vibao vya mawe vya Agano.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
yenye chetezo cha dhahabu, na sanduku la agano lililofunikwa kwa dhahabu pande zote, mlimokuwa na kopo la dhahabu lenye ile mana, na ile fimbo ya Haruni iliyochipuka, na vile vibao vya agano;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Katika Patakatifu pa Patakatifu kulikuwepo madhabahu ya dhahabu kwa ajili ya kuchoma uvumba. Pia lilikuwepo Sanduku la Agano. Sanduku lilifunikwa kwa dhahabu. Ndani ya hilo Sanduku kulikuwemo birika la mana na fimbo ya Haruni; fimbo ambayo iliwahi kuchipusha matawi. Vilevile ndani ya Sanduku yalikuwemo mawe bapa yaliyoandikwa Amri Kumi za agano la kale kwao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Humo mlikuwa na madhabahu ya dhahabu kwa ajili ya kufukizia ubani, na Sanduku la Agano, ambalo lilikuwa limepakwa dhahabu pande zote, na ndani yake mlikuwa na chungu cha dhahabu kilichokuwa na mana; fimbo ya Aroni iliyokuwa imechanua majani, na vile vibao viwili vilivyoandikwa agano.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Humo mlikuwa na madhabahu ya dhahabu kwa ajili ya kufukizia ubani, na sanduku la agano, ambalo lilikuwa limepakwa dhahabu pande zote, na ndani yake mlikuwa na chungu cha dhahabu kilichokuwa na mana, fimbo ya Aroni iliyokuwa imechanua majani, na vile vibao viwili vya mawe vilivyoandikwa agano.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
ambako ndiko kulikokuwa na ile madhabahu ya dhahabu ya kufukizia uvumba na lile Sanduku la Agano lililofunikwa dhahabu. Sanduku hili lilikuwa na gudulia la dhahabu lenye ile mana, ile fimbo ya Aroni iliyochipuka na vile vibao vya mawe vya Agano.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
ambapo palikuwa na yale madhabahu ya dhahabu ya kufukizia uvumba, na lile Sanduku la Agano lililofunikwa kwa dhahabu. Sanduku hili lilikuwa na gudulia la dhahabu lenye mana, ile fimbo ya Haruni iliyochipuka, na vile vibao vya mawe vya Agano.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
yenye chetezo cha dhahabu, na sanduku la Agano lililofunikwa kwa dhahabu pande zote, mlimokuwa na kopo la dhahabu lenye ile mana, na ile fimbo ya Haruni iliyochipuka, na vile vibao vya agano;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Humo mlikuwa na madhabahu ya dhahabu kwa ajili ya kufukizia ubani, na sanduku la agano, ambalo lilikuwa limepakwa dhahabu pande zote, na ndani yake mlikuwa na chungu cha dhahabu kilichokuwa na mana, fimbo ya Aroni iliyokuwa imechanua majani, na vile vibao viwili vya mawe vilivyoandikwa agano.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Humo mlikuwa na kivukizio cha uvumba cha dhahabu tupu na Sanduku la Agano lililofunikizwa po pote na mabati ya dhahabu; ndani yake mlikuwa na kitungi cha dhahabu chenye Mana na fimbo yake Haroni iliyochipuka na vibao vya Agano.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
yenye chetezo cha dhahabu, na sanduku la agano lililofunikwa kwa dhahabu pande zote, mlimokuwa na kopo la dhahabu lenye ile mana, na ile fimbo ya Haruni iliyochipuka, na vile vibao vya agano;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ndani ya chumba kile kulikuwa chombo cha kufukizia ubani, kilichotengenezwa na zahabu. Na kulikuwa vilevile Sanduku la Agano lililopakaliwa zahabu pande zote. Ndani ya sanduku lile kulikuwa kopo la zahabu lenye mana, na fimbo ya Haruni iliyoota vichipukizi juu yake. Kulikuwa vilevile vibao vya mawe vyenye Maandiko ya Agano la Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
yenye cheteso cha dhahabu, na sanduku ya agano iliyofunikwa kwa dhahabu pande zote, mlimokuwa na kopo la dhahabu lenye manna, na fimbo ya Haruni iliyochipuka, na vibao vya agano;