Hebrews 9:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Juu ya hilo sanduku kulikuwa na viumbe wenye mabawa, na mabawa yao yalitanda juu ya kiti cha rehema. Lakini sasa hatuwezi kusema kinaganaga juu ya mambo hayo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Juu ya lile Sanduku kulikuwa na makerubi wa Utukufu, wakikitia kivuli kiti cha rehema. Lakini hatuwezi kujadili vitu hivi kwa undani sasa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na juu yake makerubi ya utukufu, yakikitia kivuli kiti cha rehema; basi hatuna nafasi sasa ya kueleza habari za vitu hivi kimoja kimoja.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Juu ya Sanduku walikuwepo viumbe wenye mbawa walioonesha utukufu wa Mungu. Viumbe hawa wenye mbawa walikuwa juu ya sehemu ya rehema. Lakini hatuwezi kusema chochote kuhusu hili hivi sasa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Juu ya hilo Sanduku kulikuwa na viumbe vilivyodhihirisha kuweko kwa Mungu, na mabawa yao yalitanda juu ya mahali ambapo dhambi huondolewa. Lakini sasa, hatuwezi kusema kinaganaga juu ya mambo hayo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Juu ya hilo sanduku kulikuwa na viumbe wenye mabawa, na mabawa yao yalitanda juu ya kiti cha rehema. Lakini sasa hatuwezi kusema kinaganaga juu ya mambo hayo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Juu ya lile Sanduku kulikuwa na makerubi ya Utukufu yakitilia kivuli kile kifuniko ambacho ndicho kiti cha rehema. Lakini hatuwezi kueleza vitu hivi kwa undani sasa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Juu ya lile Sanduku kulikuwa na makerubi ya Utukufu yakitilia kivuli kile kifuniko ambacho ndicho kiti cha rehema. Lakini hatuwezi kueleza vitu hivi kwa undani sasa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na juu yake makerubi ya utukufu, yakikitia kivuli kiti cha rehema; basi hatuna nafasi sasa ya kueleza habari za vitu hivi kimoja kimoja.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Juu ya hilo sanduku kulikuwa na viumbe wenye mabawa, na mabawa yao yalitanda juu ya kiti cha rehema. Lakini sasa hatuwezi kusema kinaganaga juu ya mambo hayo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini juu ilikuwa imefunikwa na Makerubi yenye utukufu waliokipatia hicho Kiti cha Upozi kivuli. Hayo yote hatuwezi kuyasema sasa moja moja.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na juu yake makerubi ya utukufu, yakikitia kivuli kiti cha rehema; basi hatuna nafasi sasa ya kueleza habari za vitu hivi kimoja kimoja.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na juu ya lile sanduku kulikuwa sanamu mbili za makerubi zilizoonyesha utukufu wa Mungu. Mabawa yao yalikuwa yakinyooshwa juu ya kiti cha rehema. Lakini sasa si wakati wa kueleza mambo hayo yote moja kwa moja.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
na juu yake makerubi ya utakatifu, yakilitia kivuli kao la rehema; bassi hatuma nafasi ya kueleza khabari za vitu hivi moja moja.