Hebrews 9:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mipango hiyo ilitekelezwa, kisha ikawa desturi kwa makuhani kuingia kila siku katika hema ya nje kutoa huduma zao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi vitu hivi vilipokuwa vimepangwa, makuhani waliingia mara kwa mara katika sehemu ya kwanza ya hema ili kufanya taratibu zao za ibada.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, vitu hivi vikiisha kutengenezwa hivyo, makuhani huingia katika hema hiyo ya kwanza daima, wakiyatimiza mambo ya ibada.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kila kitu ndani ya hema kilikuwa kimewekwa tayari kwa namna nilivyoeleza. Kisha makuhani waliingia ndani ya chumba cha kwanza kila siku kutekeleza shughuli zao za ibada.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mipango hiyo ilitekelezwa kisha ikawa desturi kwa makuhani kuingia kila siku katika hema ya nje kutoa huduma zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mipango hiyo ilitekelezwa, kisha ikawa desturi kwa makuhani kuingia kila siku katika hema ya nje kutoa huduma zao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi vitu hivi vilikuwa vimepangwa, kwamba makuhani wakiingia daima katika sehemu ya kwanza ya hema ili kufanya taratibu zao za ibada,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi vitu hivi vilipokuwa vimepangwa, makuhani waliingia mara kwa mara katika sehemu ya kwanza ya hema ili kufanya taratibu zao za ibada.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, vitu hivi vikiisha kutengenezwa hivyo, makuhani huingia katika hema hiyo ya kwanza daima, wakiyatimiza mambo ya ibada.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mipango hiyo ilitekelezwa, kisha ikawa desturi kwa makuhani kuingia kila siku katika hema ya nje kutoa huduma zao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi vilipokwisha kutengenezwa hivyo, watambikaji huingia kila siku katika hema la kwanza wakifanya kazi za tambiko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, vitu hivi vikiisha kutengenezwa hivyo, makuhani huingia katika hema hiyo ya kwanza daima, wakiyatimiza mambo ya ibada.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni hivi ndivyo walivyopanga vitu vile vyote. Halafu makuhani waliingia kila siku katika kile chumba cha kwanza kwa kufanya kazi za ibada.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi, vitu hivi vikiislia kutengenezwa hivyo, makuhani huingia khema ya kwanza siku zote, wakiyatimiza mambo va ibada.