Hebrews 9:7 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini kuhani mkuu peke yake ndiye anayeingia katika lile hema la pili; naye hufanya hivyo mara moja tu kwa mwaka, na huwa amechukua damu ambayo anamtolea Mungu kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili ya makosa ya watu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ni kuhani mkuu peke yake aliyeingia ndani ya sehemu ya pili ya hema. Tena hii ilikuwa mara moja tu kwa mwaka, na hakuingia kamwe bila damu, ambayo alitoa kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili ya dhambi za watu walizotenda bila kukusudia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini katika hema hiyo ya pili kuhani mkuu huingia peke yake, mara moja kila mwaka; wala si pasipo damu, atoayo kwa ajili ya nafsi yake na kwa dhambi za kutokujua za hao watu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini ni kuhani mkuu tu aliweza kuingia kwenye chumba cha pili, na aliingia mara moja tu kwa mwaka. Pia, asingeweza kuingia ndani ya chumba hicho bila kuchukua damu pamoja naye. Aliitoa damu hiyo kwa Mungu kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili ya dhambi walizotenda watu bila kujua kwamba walikuwa wanatenda dhambi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini kuhani Mkuu peke yake ndiye anayeingia katika lile hema la pili; naye hufanya hivyo mara moja tu kwa mwaka. Anapoingia ndani huwa amechukua damu ambayo anamtolea Mungu kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili ya dhambi ambazo watu wamezitenda bila wao wenyewe kujua.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini kuhani mkuu peke yake ndiye anayeingia katika lile hema la pili; naye hufanya hivyo mara moja tu kwa mwaka, na huwa amechukua damu ambayo anamtolea Mungu kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili ya makosa ya watu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
lakini ni Kuhani Mkuu peke yake ndiye aliyeingia ndani ya sehemu ya pili ya hema, tena hii ilikuwa mara moja tu kwa mwaka, lakini si bila kuchukua damu ambayo angetoa kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili ya watu waliotenda dhambi bila kukusudia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini ni kuhani mkuu peke yake aliyeingia ndani ya sehemu ya pili ya hema. Tena hii ilikuwa mara moja tu kwa mwaka, na hakuingia kamwe bila damu, ambayo alitoa kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili ya dhambi za watu walizotenda bila kukusudia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini katika hema hiyo ya pili kuhani mkuu huingia peke yake, mara moja kila mwaka; wala si pasipo damu, atoayo kwa ajili ya nafsi yake na kwa dhambi walizozitenda hao watu bila kujua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini kuhani mkuu peke yake ndiye anayeingia katika lile hema la pili; naye hufanya hivyo mara moja tu kwa mwaka, na huwa amechukua damu ambayo anamtolea Mungu kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili ya makosa ya watu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini katika hema la pili humwingia mtambikaji mkuu peke yake kila mwaka mara moja tu, naye hamwingii pasipo damu, anayoipeleka, iwe kole yake yeye na ya makosa ya watu wanaojikosea tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini katika hema hiyo ya pili kuhani mkuu huingia peke yake, mara moja kila mwaka; wala si pasipo damu, atoayo kwa ajili ya nafsi yake na kwa dhambi za kutokujua za hao watu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini ni Kuhani Mukubwa peke yake ndiye aliyeingia katika kile chumba cha pili mara moja tu kila mwaka. Naye alipaswa kupeleka mule damu ya nyama anayotoa sadaka kwa ajili ya zambi zake mwenyewe na kwa ajili ya zambi watu walizofanya kwa kutokujua.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini katika khema ya pili kuhani mkuu huingia peke yake, marra moja killa mwaka; wala si pasipo damu, atoayo kwa ajili ya nafsi yake na dhambi za ujinga za watu.