Hebrews 9:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kutokana na taratibu hizo Roho Mtakatifu anafundisha wazi kwamba wakati ile hema ya nje ingali ipo imesimama, njia ya kuingia Mahali Patakatifu sana haijafunguliwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa njia hii, Roho wa Mungu alikuwa anaonesha kwamba, maadamu lile hema la kwanza lilikuwa bado limesimama, njia ya kuingia Patakatifu pa Patakatifu ilikuwa bado haijafunguliwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Roho Mtakatifu akionyesha neno hili, ya kwamba njia ya kupaingia patakatifu ilikuwa haijadhihirishwa bado, hapo hema ya kwanza ilipokuwa ingali ikisimama;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Roho Mtakatifu hutumia vyumba hivi viwili tofauti kutufundisha kwamba njia ya kuelekea Patakatifu pa Patakatifu haikuwa wazi wakati chumba cha kwanza kilipokuwepo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kutokana na taratibu hizo Roho Mtakatifu anafundisha wazi kwamba wakati ile hema ya nje ingali ipo imesimama, njia ya kuingia Mahali Patakatifu haijafunguliwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kutokana na taratibu hizo Roho Mtakatifu anafundisha wazi kwamba wakati ile hema ya nje ingali ipo imesimama, njia ya kuingia Mahali Patakatifu sana haijafunguliwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa njia hii, Roho Mtakatifu alikuwa anaonyesha kwamba maadamu ile hema ya kwanza ilikuwa bado imesimama, njia ya kuingia Patakatifu pa Patakafifu ilikuwa bado haijafunguliwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa njia hii, Roho wa Mwenyezi Mungu alikuwa anaonyesha kwamba, maadamu ile hema ya kwanza ilikuwa bado imesimama, njia ya kuingia Patakatifu pa Patakafifu ilikuwa bado haijafunguliwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Roho Mtakatifu akionesha neno hili, ya kwamba njia ya kupaingia patakatifu ilikuwa haijadhihirishwa bado, hapo hema ya kwanza ilipokuwa ingali ikisimama;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kutokana na taratibu hizo Roho Mtakatifu anafundisha wazi kwamba wakati ile hema ya nje ingali ipo imesimama, njia ya kuingia Mahali Patakatifu sana haijafunguliwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo Roho Mtakatifu hueleza kwamba: Njia ya kupaingilia Patakatifu Penyewe haijafunguka siku, hema la kwanza litakapokuwa likingali limesimama bado.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Roho Mtakatifu akionyesha neno hili, ya kwamba njia ya kupaingia patakatifu ilikuwa haijadhihirishwa bado, hapo hema ya kwanza ilipokuwa ingali ikisimama;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hivi Roho Mutakatifu alikuwa akionyesha kwamba njia ya kuingia katika Pahali Patakatifu Sana ilikuwa bado kufunguliwa kwa wakati wote ile Hema ya kwanza ilipokuwa ingali ikisimikwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Roho Mtakatifu akionyesha neno hili, ya kwamba njia ya kupaingia patakatifu ilikuwa haijadhihirishwa bado, hapo khema ya kwanza ilipokuwa ingali ikisimama.