Hosea 1:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Gomeri alipata mimba tena, akazaa mtoto wa kike. Mwenyezi-Mungu akamwambia Hosea, “Mpe mtoto huyo jina ‘Asiyehurumiwa’, maana sitawahurumia tena Waisraeli wala sitawasamehe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Gomeri akachukua tena mimba akamzaa binti. Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia Hosea, “Mwite Lo-Ruhama, kwa maana sitaonesha tena upendo kwa nyumba ya Israeli, kwamba nisije kabisa nikawasamehe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akachukua mimba tena, akazaa mtoto mwanamke. Bwana akamwambia, Mwite jina lake Lo-ruhama
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Gomeri alipata mimba tena, akazaa mtoto wa kike. Mwenyezi-Mungu akamwambia Hosea, “Mpe mtoto huyo jina ‘Asiyehurumiwa’, maana sitawahurumia tena Waisraeli wala sitawasamehe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Gomeri akachukua tena mimba akamzaa binti. Kisha BWANA akamwambia Hosea, “Mwite Lo-Ruhama, kwa maana sitaonyesha tena upendo kwa nyumba ya Israeli, kwamba nisije kabisa nikawasamehe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Gomeri akachukua tena mimba akamzaa binti. Kisha bwana akamwambia Hosea, “Mwite Lo-Ruhama, kwa maana sitaonyesha tena upendo kwa nyumba ya Israeli, kwamba nisije kabisa nikawasamehe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akachukua mimba tena, akazaa mtoto wa kike, BWANA akamwambia, Mwite jina lake Lo-ruhama; kwa maana sitairehemu nyumba ya Israeli tena, nisije nikawasamehe kwa njia yoyote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Gomeri alipata mimba tena, akazaa mtoto wa kike. Mwenyezi-Mungu akamwambia Hosea, “Mpe mtoto huyo jina ‘Asiyehurumiwa’, maana sitawahurumia tena Waisraeli wala sitawasamehe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akapata mimba tena, akazaa mwana wa kike. Bwana akamwambia: Mwite jina lake Hahurumiwi! Kwani sitawahurumia tena walio mlango wa Isiraeli nikiendelea kuwaondolea mabaya yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akachukua mimba tena, akazaa mtoto mwanamke. BWANA akamwambia, Mwite jina lake Lo-ruhama; kwa maana sitairehemu nyumba ya Israeli tena, nisije nikawasamehe kwa njia yo yote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Gomeri alipata mimba tena, akazaa mutoto mwanamuke. Yawe akamwambia Hosea: Umupange mutoto huyo jina la “Asiyehurumiwa”, maana sitawahurumia tena Waisraeli wala sitawasamehe.