Hosea 10:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waisraeli walikuwa kama mzabibu mzuri, mzabibu wenye kuzaa matunda. Kadiri matunda yalivyozidi kuongezeka, ndivyo walivyozidi kujijengea madhabahu. Kadiri nchi yao ilivyozidi kustawi, ndivyo walivyozidi kupamba nguzo zao za ibada.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Israeli alikuwa mzabibu uliostawi sana, alijizalia matunda mwenyewe. Kadiri matunda yake yalivyoongezeka, alijenga madhabahu zaidi; kadiri nchi yake ilivyostawi, alipamba mawe yake ya ibada.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Israeli ni mzabibu, utoao matunda yake; kwa kadiri ya wingi wa matunda yake, kwa kadiri iyo hiyo ameongeza madhabahu zake; kwa kadiri ya wema wa nchi yake, kwa kadiri iyo hiyo wamefanya nguzo nzuri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waisraeli walikuwa kama mzabibu mzuri, mzabibu wenye kuzaa matunda. Kadiri matunda yalivyozidi kuongezeka, ndivyo walivyozidi kujijengea madhabahu. Kadiri nchi yao ilivyozidi kustawi, ndivyo walivyozidi kupamba nguzo zao za ibada.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Israeli alikuwa mzabibu uliostawi sana, alijizalia matunda mwenyewe. Kadiri matunda yake yalivyoongezeka, alijenga madhabahu zaidi; kadiri nchi yake ilivyostawi, alipamba mawe yake ya ibada.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Israeli alikuwa mzabibu uliostawi sana, alijizalia matunda mwenyewe. Kadiri matunda yake yalivyoongezeka, alijenga madhabahu zaidi; kadiri nchi yake ilivyostawi, alipamba mawe yake ya ibada.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Israeli ni mzabibu mzuri, utoao matunda yake; kwa kadiri ya wingi wa matunda yake, kwa kadiri hiyo hiyo ameongeza madhabahu zake; kwa kadiri ya wema wa nchi yake, kwa kadiri hiyo hiyo wamefanya nguzo nzuri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waisraeli walikuwa kama mzabibu mzuri, mzabibu wenye kuzaa matunda. Kadiri matunda yalivyozidi kuongezeka, ndivyo walivyozidi kujijengea madhabahu. Kadiri nchi yao ilivyozidi kustawi, ndivyo walivyozidi kupamba nguzo zao za ibada.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Isiraeli ni mzabibu uchipukao vema, uzaao matunda mema; lakini kama matunda yake yalivyo mengi ndivyo, walivyojitengenezea pengi pa kutambikia, kwa wema wa nchi yako waliulinganya wema wa vinyago.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Israeli ni mzabibu, utoao matunda yake; kwa kadiri ya wingi wa matunda yake, kwa kadiri iyo hiyo ameongeza madhabahu zake; kwa kadiri ya wema wa nchi yake, kwa kadiri iyo hiyo wamefanya nguzo nzuri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waisraeli walikuwa kama muzabibu muzuri, muzabibu wenye kuzaa matunda. Kadiri matunda yalivyozidi kuongezeka, ndivyo walivyozidi kujijengea mazabahu. Kadiri inchi yao ilivyozidi kustawi, ndivyo walivyozidi kupamba nguzo zao za ibada.