Hosea 10:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Efraimu ni ndama aliyefundishwa vizuri, akapenda kupura nafaka. Lakini sasa shingo yake nzuri nitaifunga nira. Yuda atalima kwa jembe yeye mwenyewe, naam, Yakobo atakokota jembe la kupalilia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Efraimu ni ndama jike aliyefundishwa ambaye hupenda kupura; hivyo nitamfunga nira juu ya shingo yake nzuri. Nitamwendesha Efraimu, Yuda lazima alime, naye Yakobo lazima avunjavunje mabonge ya udongo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Efraimu ni ndama aliyefundishwa, apendaye kupura; lakini nimepitisha kongwa juu ya shingo yake nzuri; nitampandisha mwenye kupanda juu ya Efraimu; Yuda atalima, na Yakobo atavunja madongoa yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Efraimu ni ndama aliyefundishwa vizuri, akapenda kupura nafaka. Lakini sasa shingo yake nzuri nitaifunga nira. Yuda atalima kwa jembe yeye mwenyewe, naam, Yakobo atakokota jembe la kupalilia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Efraimu ni mtamba wa ng'ombe aliyefundishwa ambaye hupenda kupura, hivyo nitamfunga nira juu ya shingo yake nzuri. Nitamwendesha Efraimu, Yuda lazima alime, naye Yakobo lazima avunjevunje mabonge ya udongo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Efraimu ni mtamba wa ng’ombe aliyefundishwa ambaye hupenda kupura, hivyo nitamfunga nira juu ya shingo yake nzuri. Nitamwendesha Efraimu, Yuda lazima alime, naye Yakobo lazima avunjavunje mabonge ya udongo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Efraimu ni ndama aliyefundishwa, apendaye kupura; lakini nimepitisha kongwa juu ya shingo yake nzuri; nitampandisha mwenye kupanda juu ya Efraimu; Yuda atalima, na Yakobo atapiga haro yeye mwenyewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Efraimu ni ndama aliyefundishwa vizuri, akapenda kupura nafaka. Lakini sasa shingo yake nzuri nitaifunga nira. Yuda atalima kwa jembe yeye mwenyewe, naam, Yakobo atakokota jembe la kupalilia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Efuraimu anafanana na ndama aliyefundishwa, apendaye kupura; nami nitautumia uzuri wa shingo yake na kumfundisha kuvuta gari; hata Yuda atalima mahali pa ng'ombe, naye Yakobo atajipondea mwenyewe madongo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Efraimu ni ndama aliyefundishwa, apendaye kupura; lakini nimepitisha kongwa juu ya shingo yake nzuri; nitampandisha mwenye kupanda juu ya Efraimu; Yuda atalima, na Yakobo atavunja madongoa yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Efuraimu ni mwana-ngombe aliyefundishwa vizuri, akapenda kupepeta ngano. Lakini sasa shingo yake nzuri nitaifunga nira. Yuda atalima kwa jembe yeye mwenyewe, Yakobo atakokota jembe la kupalilia.