Hosea 10:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mahali pa kuabudia vilimani pa Aweni, dhambi ya Waisraeli, pataharibiwa. Miiba na magugu vitamea katika madhabahu zao. Nao wataiambia milima, “Tufunikeni” na vilima, “Tuangukieni!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mahali pa juu pa uovu pataharibiwa: ndiyo dhambi ya Israeli. Miiba na mibaruti itaota na kufunika madhabahu zao. Kisha wataiambia milima, “Tufunikeni!” na vilima, “Tuangukieni!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mahali pa Aveni palipoinuka, yaani, dhambi ya Israeli, pataharibika; mwiba na mbigili itamea juu ya madhabahu zake; nao wataiambia milima, Tusitirini; na vilima, Tuangukieni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mahali pa kuabudia vilimani pa Aweni, dhambi ya Waisraeli, pataharibiwa. Miiba na magugu vitamea katika madhabahu zao. Nao wataiambia milima, “Tufunikeni” na vilima, “Tuangukieni!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mahali pa kuabudia sanamu pa uovu pataharibiwa: ndiyo dhambi ya Israeli. Miiba na mibaruti itaota na kufunika madhabahu zao. Kisha wataiambia milima, “Tufunikeni!” na vilima, “Tuangukieni!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mahali pa kuabudia sanamu pa uovu pataharibiwa: ndiyo dhambi ya Israeli. Miiba na mibaruti itaota na kufunika madhabahu zao. Kisha wataiambia milima, “Tufunikeni!” na vilima, “Tuangukieni!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mahali pa Aveni palipoinuka, yaani, dhambi ya Israeli, pataharibika; mwiba na mbigili itamea juu ya madhabahu zake; nao wataiambia milima, Tusitirini; na vilima, Tuangukieni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mahali pa kuabudia vilimani pa Aweni, dhambi ya Waisraeli, pataharibiwa. Miiba na magugu vitamea katika madhabahu zao. Nao wataiambia milima, “Tufunikeni” na vilima, “Tuangukieni!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Navyo vilima vya Aweni vitaangamizwa, Isiraeli alikomkosea Mungu; miti yenye miiba na mibigili itakulia hapo pao pa kutambikia; ndipo, watakapoiambia milima: Tufunikeni! nayo machuguu: Tuangukieni!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mahali pa Aveni palipoinuka, yaani, dhambi ya Israeli, pataharibika; mwiba na mbigili itamea juu ya madhabahu zake; nao wataiambia milima, Tusitirini; na vilima, Tuangukieni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Pahali pa kutambikia juu ya vilima pa Aweni, pahali Waisraeli walipofanyia zambi, pataharibiwa. Miiba na michongoma vitaota katika mazabahu zao. Nao wataiambia milima: Mutufunike na vilima: Mutuangukie!