Hosea 11:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Watanifuata mimi Mwenyezi-Mungu ningurumaye kama simba; nitakaponguruma watanijia toka magharibi wakitetemeka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watamfuata Mwenyezi Mungu; atanguruma kama simba. Anaponguruma, watoto wake watakuja wakitetemeka kutoka magharibi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watakwenda kumfuata Bwana, atakayenguruma kama simba; kwa maana atanguruma, nao watoto watakuja kutoka magharibi wakitetemeka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Watanifuata mimi Mwenyezi-Mungu ningurumaye kama simba; nitakaponguruma watanijia toka magharibi wakitetemeka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watamfuata BWANA; atanguruma kama simba. Wakati angurumapo, watoto wake watakuja wakitetemeka kutoka magharibi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watamfuata bwana; atanguruma kama simba. Wakati angurumapo, watoto wake watakuja wakitetemeka kutoka magharibi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watakwenda kumfuata BWANA, atakayenguruma kama simba; kwa maana atanguruma, nao watoto watakuja kutoka magharibi wakitetemeka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Watanifuata mimi Mwenyezi-Mungu ningurumaye kama simba; nitakaponguruma watanijia toka magharibi wakitetemeka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watakuja kumtafuta Bwana, atakaponguruma kama simba; kweli atakaponguruma, ndipo, watakapokuja kwa kutetemeka wao watoto watokao upande wa baharini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watakwenda kumfuata BWANA, atakayenguruma kama simba; kwa maana atanguruma, nao watoto watakuja kutoka magharibi wakitetemeka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watanifuata mimi Yawe ninayenguruma kama simba; nitakaponguruma watanifikia toka magaribi wakitetemeka.