Hosea 12:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huko Gileadi ni mahali pa dhambi; huko Gilgali walitambika fahali, kwa hiyo madhabahu zao zitakuwa marundo ya mawe kwenye mitaro shambani.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, Gileadi si mwovu? Watu wake hawafai kitu! Je, hawatoi dhabihu za mafahali huko Gilgali? Madhabahu zao zitakuwa kama malundo ya mawe katika shamba lililolimwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Gileadi ni uovu? Wamekuwa ubatili tu; huko Gilgali hutoa dhabihu za ng'ombe; naam, madhabahu zao zimekuwa kama chungu katika matuta ya mashamba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huko Gileadi ni mahali pa dhambi; huko Gilgali walitambika fahali, kwa hiyo madhabahu zao zitakuwa marundo ya mawe kwenye mitaro shambani.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, Gileadi si mwovu? Watu wake hawafai kitu! Je, hawatoi dhabihu za mafahali huko Gilgali? Madhabahu zao zitakuwa kama malundo ya mawe katika shamba lililolimwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, Gileadi si mwovu? Watu wake hawafai kitu! Je, hawatoi dhabihu za mafahali huko Gilgali? Madhabahu zao zitakuwa kama malundo ya mawe katika shamba lililolimwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika Gileadi kuna uovu? Nao wamekuwa ubatili tu; huko Gilgali hutoa dhabihu za ng'ombe; naam, madhabahu zao zimekuwa kama chungu katika matuta ya mashamba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huko Gileadi ni mahali pa dhambi; huko Gilgali walitambika fahali, kwa hiyo madhabahu zao zitakuwa marundo ya mawe kwenye mitaro shambani.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mimi nilisema na wafumbuaji, nikawatokea mara nyingi, nikawaonya kwa vinywa vya wafumbuaji na kusema mifano.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Gileadi ni uovu? Wamekuwa ubatili tu; huko Gilgali hutoa dhabihu za ng’ombe; naam, madhabahu zao zimekuwa kama chungu katika matuta ya mashamba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi niliongea na manabii; ni mimi niliyewapa maono mengi, na kwa njia yao nilitangaza mupango wangu.