Hosea 12:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu asema, “Mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mungu wako; mimi ndimi niliyekutoa nchini Misri! Mimi nitakukalisha tena katika mahema, kama ufanyavyo sasa kwa siku chache tu, wakati wa sikukuu ya vibanda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, niliyewaleta kutoka Misri; nitawafanya mkae tena kwenye mahema, kama vile katika siku za sikukuu zenu zilizoamriwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini mimi ni Bwana, Mungu wako tangu ulipotoka katika nchi ya Misri; nitakukalisha tena katika hema, kama siku za karamu ya idi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu asema, “Mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mungu wako; mimi ndimi niliyekutoa nchini Misri! Mimi nitakukalisha tena katika mahema, kama ufanyavyo sasa kwa siku chache tu, wakati wa sikukuu ya vibanda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mimi ndimi BWANA Mungu wenu niliyewaleta kutoka Misri; nitawafanya mkae tena kwenye mahema, kama vile katika siku za sikukuu zenu zilizoamuriwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mimi ndimi bwana Mwenyezi Mungu wenu niliyewaleta kutoka Misri; nitawafanya mkae tena kwenye mahema, kama vile katika siku za sikukuu zenu zilizoamriwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini mimi ni BWANA, Mungu wako tangu ulipotoka katika nchi ya Misri; nitakukalisha tena katika hema, kama siku za sikukuu teule.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu asema, “Mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mungu wako; mimi ndimi niliyekutoa nchini Misri! Mimi nitakukalisha tena katika mahema, kama ufanyavyo sasa kwa siku chache tu, wakati wa sikukuu ya vibanda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Efuraimu husema: Kumbe ni tajiri! Nimejipatia mali! Tena kwa hivyo vyote, nilivyovisumbukia, hawataniona, ya kuwa nimefanya kiovu cha kumkosea mtu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini mimi ni BWANA, Mungu wako tangu ulipotoka katika nchi ya Misri; nitakukalisha tena katika hema, kama siku za karamu ya idi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Efuraimu amesema: Mimi ni tajiri! Mimi nimejitajirisha! Sikufanya mabaya kwa kupata hii faida.