Hosea 13:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yanibidi kuwakomboa hawa watu kutoka kuzimu; sharti niwaokoe kutoka kifoni! Ewe Kifo, yako wapi maafa yako? Ewe Kuzimu, yako wapi maangamizi yako? Mimi sitawaonea tena huruma!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Nitawakomboa watu hawa kutoka nguvu za kaburi, nitawakomboa kutoka mautini. Yako wapi, ee mauti, mateso yako? Uko wapi, ee Kuzimu, uharibifu wako? “Sitakuwa na huruma,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nitawakomboa na nguvu za kaburi; nitawaokoa na mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi, ku wapi kuharibu kwako? Kujuta kutafichwa na macho yangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yanibidi kuwakomboa hawa watu kutoka kuzimu; sharti niwaokoe kutoka kifoni! Ewe Kifo, yako wapi maafa yako? Ewe Kuzimu, yako wapi maangamizi yako? Mimi sitawaonea tena huruma!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Nitawakomboa watu hawa kutoka nguvu za kaburi, nitawakomboa kutoka mautini. Yako wapi, Ee mauti, mateso yako? Uko wapi, Ee kuzimu, uharibifu wako? “Sitakuwa na huruma,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Nitawakomboa watu hawa kutoka nguvu za kaburi, nitawakomboa kutoka mautini. Yako wapi, ee mauti, mateso yako? Uko wapi, ee kuzimu, uharibifu wako? “Sitakuwa na huruma,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nitawakomboa kwa nguvu za kaburi; nitawaokoa kutoka kwa mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi, ku wapi kuharibu kwako? Huruma itafichika machoni mwangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yanibidi kuwakomboa hawa watu kutoka kuzimu; sharti niwaokoe kutoka kifoni! Ewe Kifo, yako wapi maafa yako? Ewe Kuzimu, yako wapi maangamizi yako? Mimi sitawaonea tena huruma!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nitawakomboa katika nguvu za kuzimuni na kuwaokoa kufani. Wewe Kifo, magonjwa yako yauayo yako wapi? Wewe Kuzimu, uchungu wako uko wapi? Ndipo, yawezayo kujutisha yatakapokuwa yamefichwa, macho yangu yasiyaone.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nitawakomboa na nguvu za kaburi; nitawaokoa na mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi, ku wapi kuharibu kwako? Kujuta kutafichwa na macho yangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Inanipasa kuwakomboa hawa watu kutoka kuzimu; sharti niwaokoe kutoka kifo! Ewe kifo, mapigo yako ni wapi? Ewe kuzimu, kuangamiza kwako ni wapi? Mimi sitawaonea tena huruma!