Hosea 13:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, watatoweka kama ukungu wa asubuhi, kama umande utowekao upesi; kama makapi yanayopeperushwa mahali pa kupuria, kama moshi unaotoka katika bomba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo watakuwa kama ukungu wa asubuhi, kama umande wa alfajiri utowekao, kama makapi yapeperushwayo kutoka sakafu ya kupuria nafaka, kama moshi utorokao kupitia dirishani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu hiyo watakuwa kama wingu la asubuhi, na kama umande utowekao upesi, kama makapi yaliyopeperushwa na tufani sakafuni, na kama moshi utokao katika bomba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, watatoweka kama ukungu wa asubuhi, kama umande utowekao upesi; kama makapi yanayopeperushwa mahali pa kupuria, kama moshi unaotoka katika bomba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo watakuwa kama ukungu wa asubuhi, kama umande wa alfajiri utowekao, kama makapi yapeperushwayo kutoka katika sakafu ya kupuria nafaka, kama moshi utorokao kupitia dirishani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo watakuwa kama ukungu wa asubuhi, kama umande wa alfajiri utowekao, kama makapi yapeperushwayo kutoka sakafu ya kupuria nafaka, kama moshi utorokao kupitia dirishani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu hiyo watakuwa kama wingu la asubuhi, na kama umande utowekao upesi, kama makapi yaliyopeperushwa na tufani sakafuni, na kama moshi utokao katika bomba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, watatoweka kama ukungu wa asubuhi, kama umande utowekao upesi; kama makapi yanayopeperushwa mahali pa kupuria, kama moshi unaotoka katika bomba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa sababu hiyo watakuwa kama wingu la asubuhi na kama umande ukaukao upesi, au kama makapi yanayopeperushwa penye kupuria au kama moshi utokao katika bomba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu hiyo watakuwa kama wingu la asubuhi, na kama umande utowekao upesi, kama makapi yaliyopeperushwa na tufani sakafuni, na kama moshi utokao katika bomba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, watatoweka kama ukungu wa asubui, kama umande unaotoweka upesi; kama makapi yanayopeperushwa kwenye nafasi ya kupepetea, kama moshi unaotoka katika munara wa kutoshea moshi inje.