Hosea 14:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Enyi Waisraeli, mrudieni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Mmejikwaa kwa sababu ya uovu wenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Rudi, ee Israeli, kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wako. Dhambi zako zimekuwa anguko lako!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ee Israeli, mrudie Bwana, Mungu wako; maana umeanguka kwa sababu ya uovu wako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wa Samaria wataadhibiwa kwa kosa lao. Kwa sababu wamemwasi Mungu wao. Watauawa kwa upanga, vitoto vyao vitapondwapondwa, na kina mama wajawazito watatumbuliwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Rudi, Ee Israeli, kwa BWANA Mungu wako. Dhambi zako zimekuwa ndilo anguko lako!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Rudi, ee Israeli, kwa bwana Mwenyezi Mungu wako. Dhambi zako zimekuwa ndilo anguko lako!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ee Israeli, mrudie BWANA, Mungu wako; maana umeanguka kwa sababu ya uovu wako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Enyi Waisraeli, mrudieni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Mmejikwaa kwa sababu ya uovu wenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Samaria atalipishwa manza, alizozikora kwa kumpingia Mungu wake: kwa hiyo wataangushwa kwa panga, watoto wao wachanga watapondwa, nao wanawake wenye mimba watatumbuliwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ee Israeli, mrudie BWANA, Mungu wako; maana umeanguka kwa sababu ya uovu wako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wa Samaria wataazibiwa kwa ajili ya kosa lao; wamemwasi Mungu wao. Watauawa kwa upanga, watoto wao watapondwapondwa, na wamama wenye mimba watapasuliwa tumbo.