Hosea 14:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Chipukizi zao zitatanda na kuenea, uzuri wao utakuwa kama mizeituni, harufu yao nzuri kama maua ya Lebanoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
matawi yake yatatanda. Fahari yake itakuwa kama mti wa mzeituni, harufu yake nzuri kama mwerezi wa Lebanoni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Matawi yake yatatandaa, na uzuri wake utakuwa kama uzuri wa mzeituni, na harufu yake kama Lebanoni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitakuwa kama umande kwa Waisraeli nao watachanua kama yungiyungi, watakuwa na mizizi kama mwerezi wa Lebanoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
matawi yake yatatanda. Fahari yake itakuwa kama mti wa mzeituni, harufu yake nzuri kama mwerezi wa Lebanoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
matawi yake yatatanda. Fahari yake itakuwa kama mti wa mzeituni, harufu yake nzuri kama mwerezi wa Lebanoni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Matawi yake yatatanda, na uzuri wake utakuwa kama uzuri wa mzeituni, na harufu yake kama Lebanoni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Chipukizi zao zitatanda na kuenea, uzuri wao utakuwa kama mizeituni, harufu yao nzuri kama maua ya Lebanoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, nitakapokuwa kwake Isiraeli kama umande, apate kuchanua kama maua ya shambani, ashushe mizizi yake kama miti ya Libanoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Matawi yake yatatandaa, na uzuri wake utakuwa kama uzuri wa mzeituni, na harufu yake kama Lebanoni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitakuwa kama umande kwa Waisraeli nao watachanua kama mayungiyungi, watakuwa na mizizi kama muti wa mwerezi wa Lebanoni.