Hosea 14:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yeyote aliye na hekima ayaelewe mambo haya, mtu aliye na busara ayatambue. Maana njia za Mwenyezi-Mungu ni nyofu; watu wanyofu huzifuata, lakini wakosefu hujikwaa humo.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ni nani mwenye hekima? Atayatambua mambo haya. Ni nani mwenye ufahamu? Huyu atayaelewa. Njia za Mwenyezi Mungu ni adili; wenye haki huenda katika njia hizo, lakini waasi watajikwaa ndani yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ni nani aliye na hekima, naye atayafahamu mambo haya? Ni nani aliye na busara, naye atayajua? Kwa maana njia za Bwana zimenyoka, nao wenye haki watakwenda katika njia hizo; bali waasio wataanguka ndani yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Enyi watu wa Efraimu, mna haja gani tena na sanamu? Mimi ndiye ninayesikiliza sala zenu, mimi ndiye ninayewatunzeni. Mimi nitawapa kivuli kama mberoshi, kutoka kwangu mtapata matunda yenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ni nani mwenye hekima? Atayatambua mambo haya. Ni nani mwenye ufahamu? Huyu atayaelewa. Njia za BWANA ni adili; wenye haki huenda katika njia hizo, lakini waasi watajikwaa ndani yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ni nani mwenye hekima? Atayatambua mambo haya. Ni nani mwenye ufahamu? Huyu atayaelewa. Njia za bwana ni adili; wenye haki huenda katika njia hizo, lakini waasi watajikwaa ndani yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ni nani aliye na hekima, naye atayafahamu mambo haya? Ni nani aliye na busara, naye atayajua? Kwa maana njia za BWANA zimenyoka, nao wenye haki watakwenda katika njia hizo; bali waasio wataanguka ndani yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yeyote aliye na hekima ayaelewe mambo haya, mtu aliye na busara ayatambue. Maana njia za Mwenyezi-Mungu ni nyofu; watu wanyofu huzifuata, lakini wakosefu hujikwaa humo.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Efuraimu atakaposema: Vinyago vinanifaliaje tena? Nami nitamjibu na kumtazama kwa kupendezwa: Mimi ni kama mvinje mbichi, kwangu mimi kutaonekana yaliyo mazao yako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ni nani aliye na hekima, naye atayafahamu mambo haya? Ni nani aliye na busara, naye atayajua? Kwa maana njia za BWANA zimenyoka, nao wenye haki watakwenda katika njia hizo; bali waasio wataanguka ndani yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Enyi watu wa Efuraimu, muko na maneno gani tena na sanamu? Mimi ndiye ninayesikiliza maombi yenu, mimi ndiye ninayewatunza. Mimi nitawapa kivuli kama cha muti wa muberoshi; kutoka kwangu mutapata matunda yenu.