Hosea 2:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo wakati wa mavuno nitaichukua nafaka yangu, nitaiondoa divai yangu wakati wake. Nitamnyang'anya nguo zangu za sufu na kitani, ambazo zilitumika kuufunika uchi wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kwa hiyo nitachukua nafaka yangu wakati itakapokomaa na divai yangu mpya wakati itakapokuwa tayari. Nitamnyang’anya sufu yangu na kitani yangu iliyokusudiwa kufunika uchi wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi kwa ajili ya hayo, nitaitwaa tena ngano yangu kwa wakati wake, na divai yangu kwa wakati wake, nami nitamnyang'anya sufu yangu na kitani yangu, vya kumfunika uchi wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo wakati wa mavuno nitaichukua nafaka yangu, nitaiondoa divai yangu wakati wake. Nitamnyang'anya nguo zangu za sufu na kitani, ambazo zilitumika kuufunika uchi wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kwa hiyo nitachukua nafaka yangu wakati itakapokomaa na divai yangu mpya wakati itakapokuwa tayari. Nitamnyang'anya sufu yangu na kitani yangu iliyokusudiwa kufunika uchi wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kwa hiyo nitachukua nafaka yangu wakati itakapokomaa na divai yangu mpya wakati itakapokuwa tayari. Nitamnyang’anya sufu yangu na kitani yangu iliyokusudiwa kufunika uchi wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi kwa ajili ya hayo, nitaitwaa tena ngano yangu kwa wakati wake, na divai yangu kwa wakati wake, nami nitamnyang'anya sufu yangu na kitani yangu, vya kumfunika uchi wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo wakati wa mavuno nitaichukua nafaka yangu, nitaiondoa divai yangu wakati wake. Nitamnyang'anya nguo zangu za sufu na kitani, ambazo zilitumika kuufunika uchi wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo na nirudi kuzichukua ngano zangu, siku zitakapotimia, nazo pombe zangu, pangu patakapotimia, nitampokonya nguo zangu za manyoya ya kondoo na za pamba, alizo nazo za kuufunika uchi wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi kwa ajili ya hayo, nitaitwaa tena ngano yangu kwa wakati wake, na divai yangu kwa wakati wake, nami nitamnyang’anya sufu yangu na kitani yangu, vya kumfunika uchi wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Atawafuata wapenzi wake, lakini hatawapata; atawatafuta, lakini hatawaona. Kwa hiyo atasema: Nitarudi kwa mume wangu wa kwanza; maana zamani nilikuwa na raha kuliko sasa.