Hosea 3:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baadaye, Waisraeli watarudi na kumtafuta Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, na kumtafuta mfalme wao, mzawa wa Daudi. Ndipo watakapomcha Mwenyezi-Mungu, na kutazamia wema wake siku za mwisho.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baadaye Waisraeli watarudi na kumtafuta Mwenyezi Mungu, Mungu wao, na Daudi mfalme wao. Watakuja wakitetemeka kwa Mwenyezi Mungu na kwa baraka zake katika siku za mwisho.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
baada ya hayo wana wa Israeli watarejea, na kumtafuta Bwana, Mungu wao, na Daudi, mfalme wao; nao watamwendea Bwana na wema wake kwa kicho siku za mwisho.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baadaye, Waisraeli watarudi na kumtafuta Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, na kumtafuta mfalme wao, mzawa wa Daudi. Ndipo watakapomcha Mwenyezi-Mungu, na kutazamia wema wake siku za mwisho.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baadaye Waisraeli watarudi na kumtafuta BWANA Mungu wao na Daudi mfalme wao. Watakuja wakitetemeka kwa BWANA na kwa baraka zake katika siku za mwisho.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baadaye Waisraeli watarudi na kumtafuta bwana Mwenyezi Mungu wao na Daudi mfalme wao. Watakuja wakitetemeka kwa bwana na kwa baraka zake katika siku za mwisho.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
baada ya hayo wana wa Israeli watarejea, na kumtafuta BWANA, Mungu wao, na Daudi, mfalme wao; nao watamwendea BWANA na wema wake kwa kicho siku za mwisho.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baadaye, Waisraeli watarudi na kumtafuta Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, na kumtafuta mfalme wao, mzawa wa Daudi. Ndipo watakapomcha Mwenyezi-Mungu, na kutazamia wema wake siku za mwisho.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wana wa Isiraeli watarudi, wamtafute Bwana Mungu wao na Dawidi, mfalme wao; siku zitakazokuwa za mwisho watamwendea Bwana na wema wake kwa kutetemeka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
baada ya hayo wana wa Israeli watarejea, na kumtafuta BWANA, Mungu wao, na Daudi, mfalme wao; nao watamwendea BWANA na wema wake kwa kicho siku za mwisho.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyuma, Waisraeli watarudi na kumutafuta Yawe, Mungu wao, na kumutafuta mufalme wao, wa uzao wa Daudi. Halafu watamutii Yawe, na kutazamia wema wake siku za mwisho.