Hosea 4:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Msikilizeni Mwenyezi-Mungu, enyi Waisraeli. Mwenyezi-Mungu anawashutumu wakazi wa nchi hii. “Hamna tena uaminifu wala wema nchini; hamna anayemjua Mungu katika nchi hii.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sikieni neno la Mwenyezi Mungu, enyi Waisraeli, kwa sababu Mwenyezi Mungu analo shtaka dhidi yenu ninyi mnaoishi katika nchi: “Hakuna uaminifu, hakuna upendo, hakuna kumjua Mungu katika nchi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lisikieni neno la Bwana, enyi wana wa Israeli; kwa maana Bwana ana mateto nao wakaao katika nchi, kwa sababu hapana kweli, wala fadhili, wala kumjua Mungu katika nchi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Msikilizeni Mwenyezi-Mungu, enyi Waisraeli. Mwenyezi-Mungu anawashutumu wakazi wa nchi hii. “Hamna tena uaminifu wala wema nchini; hamna anayemjua Mungu katika nchi hii.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sikieni neno la BWANA, enyi Waisraeli, kwa sababu BWANA analo shtaka dhidi yenu ninyi mnaoishi katika nchi: “Hakuna uaminifu, hakuna upendo, hakuna kumjua Mungu katika nchi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sikieni neno la bwana, enyi Waisraeli, kwa sababu bwana analo shtaka dhidi yenu ninyi mnaoishi katika nchi: “Hakuna uaminifu, hakuna upendo, hakuna kumjua Mungu katika nchi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lisikieni neno la BWANA, enyi wana wa Israeli; kwa maana BWANA ana shutuma nao wakaao katika nchi, kwa sababu hapana kweli, wala fadhili, wala kumjua Mungu katika nchi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Msikilizeni Mwenyezi-Mungu, enyi Waisraeli. Mwenyezi-Mungu anawashutumu wakazi wa nchi hii. “Hamna tena uaminifu wala wema nchini; hamna anayemjua Mungu katika nchi hii.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
lisikieni neno la Bwana, ninyi wana wa Isiraeli! Kwani Bwana yuko na neno la kuwagombeza wakaao katika nchi hii, kwa kuwa hakuna welekevu wala huruma, wala ujuzi wa Mungu katika nchi hii.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lisikieni neno la BWANA, enyi wana wa Israeli; kwa maana BWANA ana mateto nao wakaao katika nchi, kwa sababu hapana kweli, wala fadhili, wala kumjua Mungu katika nchi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musikilize maneno ya Yawe, enyi Waisraeli. Yawe anawashitaki wakaaji wa inchi hii. Hakuna tena uaminifu wala wema katika inchi; hakuna anayemujua Mungu katika inchi hii.