Hosea 4:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Ama kweli nyinyi Waisraeli ni wazinzi! Lakini, msiwafanye watu wa Yuda wawe na hatia! Msiende mahali patakatifu huko Gilgali, wala msiende kule Beth-aveni. Wala msiape mkisema, ‘Kama Mwenyezi-Mungu aishivyo!’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ingawa umefanya uzinzi, ee Israeli, Yuda naye asije akawa na hatia. “Usiende Gilgali, usipande kwenda Beth-Aveni. Wala usiape, ‘Hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo!’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ingawa wewe, Israeli, unafanya uzinzi, lakini asiasi Yuda; nanyi msiende Gilgali wala msipande mpaka Beth-Aveni, wala msiape mkisema, Aishivyo Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Ama kweli nyinyi Waisraeli ni wazinzi! Lakini, msiwafanye watu wa Yuda wawe na hatia! Msiende mahali patakatifu huko Gilgali, wala msiende kule Beth-aveni. Wala msiape mkisema, ‘Kama Mwenyezi-Mungu aishivyo!’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ingawa umefanya uzinzi, Ee Israeli, Yuda naye asije akawa na hatia. “Usiende Gilgali, usipande kwenda Beth-Aveni. Wala usiape, ‘Hakika kama BWANA aishivyo!’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ingawa umefanya uzinzi, ee Israeli, Yuda naye asije akawa na hatia. “Usiende Gilgali, usipande kwenda Beth-Aveni Wala usiape, ‘Hakika kama bwana aishivyo!’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ingawa wewe, Israeli, unafanya uzinzi, lakini asiasi Yuda; nanyi msiende Gilgali wala msipande mpaka Beth-aveni, wala msiape mkisema, Aishivyo BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Ama kweli nyinyi Waisraeli ni wazinzi! Lakini, msiwafanye watu wa Yuda wawe na hatia! Msiende mahali patakatifu huko Gilgali, wala msiende kule Beth-aveni. Wala msiape mkisema, ‘Kama Mwenyezi-Mungu aishivyo!’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wewe Isiraeli, ukiwa unafanya ugoni, usimkoseshe Yuda! Msije Gilgali! Wala msipande kwenda Beti-Aweni! Wala msiape na kusema: Hivyo, Bwana alivyo Mwenye uzima!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ingawa wewe, Israeli, unafanya uzinzi, lakini asiasi Yuda; nanyi msiende Gilgali wala msipande mpaka Beth-Aveni, wala msiape mkisema, Aishivyo BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ikiwa kweli ninyi Waisraeli ni wazinzi lakini, watu wa Yuda basi wasianguke ndani ya makosa! Musiende pahali patakatifu kule Gilgali, wala musiende kule Nyumba ya Uovu. Wala musiape mukisema: Kama vile Yawe anavyoishi!