Hosea 4:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waisraeli ni wakaidi kama punda. Kwa nini basi Mungu ashughulike kuwachunga, kama kondoo kwenye malisho mapana?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waisraeli ni wakaidi, kama ndama jike mkaidi. Ni jinsi gani basi Mwenyezi Mungu anaweza kuwachunga kama wana-kondoo katika shamba la majani?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana Israeli ametenda kwa ukaidi, kama ndama mkaidi; sasa je! Bwana atawalisha kama mwana-kondoo katika mahali penye nafasi!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waisraeli ni wakaidi kama punda. Kwa nini basi Mungu ashughulike kuwachunga, kama kondoo kwenye malisho mapana?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waisraeli ni wakaidi, kama mtamba wa ng'ombe ambaye ni mkaidi. Ni jinsi gani basi BWANA anaweza kuwachunga kama wana-kondoo katika shamba la majani?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waisraeli ni wakaidi, kama mtamba wa ng’ombe ambaye ni mkaidi. Ni jinsi gani basi bwana anaweza kuwachunga kama wana-kondoo katika shamba la majani?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana Israeli ametenda kwa ukaidi, kama ndama mkaidi; sasa je! BWANA atawalisha kama mwana-kondoo katika mahali penye malisho mazuri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waisraeli ni wakaidi kama punda. Kwa nini basi Mungu ashughulike kuwachunga, kama kondoo kwenye malisho mapana?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikiwa Isiraeli ameshupaa vibaya kama ndama wenye ushupavu, je? Bwana atamchunga kama kondoo penye lisho pana?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana Israeli ametenda kwa ukaidi, kama ndama mkaidi; sasa je! BWANA atawalisha kama mwana-kondoo katika mahali penye nafasi!
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waisraeli ni wenye kichwa kigumu kama punda. Kwa nini basi Mungu ashugulike na kuwachunga, kama kondoo katika shamba kubwa la kuwakulishia?