Hosea 5:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Haya! Sikilizeni enyi makuhani! Tegeni sikio, enyi Waisraeli! Sikilizeni enyi ukoo wa kifalme! Nyinyi mlipaswa kuzingatia haki, badala yake mmekuwa mtego huko Mizpa, mmekuwa wavu wa kuwanasa huko Tabori.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Sikieni hili, enyi makuhani! Kuweni wasikivu, enyi Waisraeli! Sikieni, ee nyumba ya mfalme! Hukumu hii ni dhidi yenu: Mmekuwa mtego huko Mispa, wavu uliotandwa juu ya Tabori.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sikieni haya, enyi makuhani, sikilizeni, enyi nyumba ya Israeli, tegeni masikio yenu, enyi wa nyumba ya mfalme, kwa kuwa hukumu hii yawahusu ninyi; maana mmekuwa mtego huko Mizpa, na wavu uliotandwa juu ya Tabori.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Haya! Sikilizeni enyi makuhani! Tegeni sikio, enyi Waisraeli! Sikilizeni enyi ukoo wa kifalme! Nyinyi mlipaswa kuzingatia haki, badala yake mmekuwa mtego huko Mizpa, mmekuwa wavu wa kuwanasa huko Tabori.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Sikieni hili, enyi makuhani! Iweni wasikivu, enyi Waisraeli! Sikieni, Ee nyumba ya kifalme! Hukumu hii ni dhidi yenu: Mmekuwa mtego huko Mizpa, wavu uliotandwa juu ya Tabori.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Sikieni hili, enyi makuhani! Kuweni wasikivu, enyi Waisraeli! Sikieni, ee nyumba ya mfalme! Hukumu hii ni dhidi yenu: Mmekuwa mtego huko Mispa, wavu uliotandwa juu ya Tabori.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sikieni haya, enyi makuhani, sikilizeni, enyi nyumba ya Israeli, tegeni masikio yenu, enyi wa nyumba ya mfalme, kwa kuwa hukumu hii yawahusu ninyi; maana mmekuwa mtego huko Mizpa, na wavu uliotandwa juu ya Tabori.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Haya! Sikilizeni enyi makuhani! Tegeni sikio, enyi Waisraeli! Sikilizeni enyi ukoo wa kifalme! Nyinyi mlipaswa kuzingatia haki, badala yake mmekuwa mtego huko Mizpa, mmekuwa wavu wa kuwanasa huko Tabori.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yasikieni haya, ninyi watambikaji! Yasikilizeni, nanyi mlio mlango wa Isiraeli! Nanyi wa mlango wa mfalme, yategeni masikio! Kwani liko shauri linalowataka, kwa maana mmekuwa tanzi la kuwanasa Wamisipa na wavu uliotegwa Tabori juu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sikieni haya, enyi makuhani, sikilizeni, enyi nyumba ya Israeli, tegeni masikio yenu, enyi wa nyumba ya mfalme, kwa kuwa hukumu hii yawahusu ninyi; maana mmekuwa mtego huko Mizpa, na wavu uliotandwa juu ya Tabori.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musikilize, enyi makuhani! Mutege sikio, enyi Waisraeli! Musikilize, enyi ukoo wa kifalme! Ninyi mulipaswa kulinda haki, pahali pake mumekuwa kama mutego kule Misipa, mumekuwa kama wavu wa kuwanasa kule Tabori.