Hosea 5:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wa Efraimu walipogundua ugonjwa wao, naam, watu wa Yuda walipogundua donda lao, watu wa Efraimu walikwenda Ashuru kuomba msaada kwa mfalme mkuu; lakini yeye hakuweza kuwatibu, hakuweza kuponya donda lenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Efraimu alipoona ugonjwa wake, naye Yuda vidonda vyake, ndipo Efraimu aligeukia Ashuru, na kuomba msaada kwa mfalme mkuu. Lakini hawezi kukuponya, hawezi kukuponya vidonda vyako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Efraimu alipouona ugonjwa wake, na Yuda jeraha yake, ndipo Efraimu alipokwenda kwa Ashuru, akatuma watu kwa mfalme Yarebu; lakini yeye hawezi kuwapoza, wala hatawaponya jeraha yenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wa Efraimu walipogundua ugonjwa wao, naam, watu wa Yuda walipogundua donda lao, watu wa Efraimu walikwenda Ashuru kuomba msaada kwa mfalme mkuu; lakini yeye hakuweza kuwatibu, hakuweza kuponya donda lenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Wakati Efraimu alipoona ugonjwa wake, naye Yuda vidonda vyake, ndipo Efraimu alipogeukia Ashuru, na kuomba msaada kwa mfalme mkuu. Lakini hawezi kukuponya, wala hawezi kukuponya vidonda vyako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Wakati Efraimu alipoona ugonjwa wake, naye Yuda vidonda vyake, ndipo Efraimu alipogeukia Ashuru, na kuomba msaada kwa mfalme mkuu. Lakini hawezi kukuponya, wala hawezi kukuponya vidonda vyako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Efraimu alipouona ugonjwa wake, na Yuda jeraha lake, ndipo Efraimu alipokwenda kwa Ashuru, akatuma watu kwa mfalme Yarebu; lakini yeye hawezi kuwapoza, wala hatawaponya jeraha lenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wa Efraimu walipogundua ugonjwa wao, naam, watu wa Yuda walipogundua donda lao, watu wa Efraimu walikwenda Ashuru kuomba msaada kwa mfalme mkuu; lakini yeye hakuweza kuwatibu, hakuweza kuponya donda lenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Efuraimu alipouona ugonjwa wake, Yuda naye alipouona usaha wa madonda yake, ndipo, Efuraimu alipokwenda Asuri, naye akatuma kwa mfalme Yarevu (Mgombeaji), lakini hataweza kuwaponya, wala hataukausha usaha wenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Efraimu alipouona ugonjwa wake, na Yuda jeraha yake, ndipo Efraimu alipokwenda kwa Ashuru, akatuma watu kwa mfalme Yarebu; lakini yeye hawezi kuwapoza, wala hatawaponya jeraha yenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wa Efuraimu walipogundua ugonjwa wao, watu wa Yuda walipogundua kidonda chao, watu wa Efuraimu walikwenda Asuria kuomba musaada kwa mufalme mukubwa; lakini yeye hakuweza kuwatunza, hakuweza kuponyesha kidonda chao.