Hosea 6:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi tumtambue, tujitahidi kumjua Mwenyezi-Mungu. Kuja kwake ni hakika kama alfajiri, yeye atatujia kama manyunyu, kama mvua za masika ziinyweshayo ardhi.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tumkubali Mwenyezi Mungu, tukaze kumkubali yeye. Kutokea kwake ni hakika kama vile kuchomoza kwa jua; atatujia kama mvua za masika, kama vile mvua za vuli ziinyweshavyo nchi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nasi na tujue, naam, tukaendelee kumjua Bwana; kutokea kwake ni yakini kama asubuhi; naye atatujilia kama mvua, kama mvua ya vuli iinyweshayo nchi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi tumtambue, tujitahidi kumjua Mwenyezi-Mungu. Kuja kwake ni hakika kama alfajiri, yeye atatujia kama manyunyu, kama mvua za masika ziinyweshayo ardhi.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tumkubali BWANA, tukaze kumkubali yeye. Kutokea kwake ni hakika kama vile kuchomoza kwa jua; atatujia kama mvua za masika, kama vile mvua za vuli ziinyweshavyo nchi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tumkubali bwana, tukaze kumkubali yeye. Kutokea kwake ni hakika kama vile kuchomoza kwa jua; atatujia kama mvua za masika, kama vile mvua za vuli ziinyweshavyo nchi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nasi na tujue, naam, tukaendelee kumjua BWANA; kutokea kwake ni yakini kama asubuhi; naye atatujia kama mvua, kama mvua ya vuli iinyweshayo nchi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi tumtambue, tujitahidi kumjua Mwenyezi-Mungu. Kuja kwake ni hakika kama alfajiri, yeye atatujia kama manyunyu, kama mvua za masika ziinyweshayo ardhi.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ndipo, tutakapojua maana, tujihimize kumjua Bwana; hana budi kutokea, kama mapambazuko yasivyokuwa na budi kutokea; atatujia kama mvua, kama mvua ya vuli inyweshayo nchi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nasi na tujue, naam, tukaendelee kumjua BWANA; kutokea kwake ni yakini kama asubuhi; naye atatujilia kama mvua, kama mvua ya vuli iinyweshayo nchi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi tumutambue, tujikaze sana kumujua Yawe. Kuja kwake ni hakika kama mapambazuko, yeye atatufikia kama vile manyunyu, kama vile mvua za kwanza zinavyolowanisha udongo.