Hosea 7:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila nikitaka kuwarekebisha watu wangu, ninapotaka kuwaponya Waisraeli, uovu wa watu wa Efraimu hufunuliwa, matendo mabaya ya Samaria hujitokeza. Wao huongozwa na udanganyifu, kwenye nyumba wezi huvunja nje barabarani wanyang'anyi huvamia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kila mara nilipotaka kumponya Israeli, dhambi za Efraimu zinafichuliwa na maovu ya Samaria yanafunuliwa. Wanafanya udanganyifu, wezi huvunja nyumba, maharamia hunyang’anya barabarani,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakati nitakapo kumponya Israeli, ndipo yafunuliwapo maovu ya Efraimu, na ubaya wa Samaria; maana wanatenda uongo, na mwivi huvunja nyumba za watu, na kundi la wanyang'anyi hushambulia nje.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila nikitaka kuwarekebisha watu wangu, ninapotaka kuwaponya Waisraeli, uovu wa watu wa Efraimu hufunuliwa, matendo mabaya ya Samaria hujitokeza. Wao huongozwa na udanganyifu, kwenye nyumba wezi huvunja nje barabarani wanyang'anyi huvamia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kila mara nilipotaka kumponya Israeli, dhambi za Efraimu zinafichuliwa na maovu ya Samaria yanafunuliwa. Wanafanya udanganyifu, wevi huvunja nyumba, maharamia hunyang'anya barabarani,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kila mara nilipotaka kumponya Israeli, dhambi za Efraimu zinafichuliwa na maovu ya Samaria yanafunuliwa. Wanafanya udanganyifu, wevi huvunja nyumba, maharamia hunyang’anya barabarani,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakati nitakapo kumponya Israeli, ndipo yafunuliwapo maovu ya Efraimu, na ubaya wa Samaria; maana wanatenda uongo, na mwizi huvunja nyumba za watu, na kundi la wanyang'anyi hushambulia nje.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila nikitaka kuwarekebisha watu wangu, ninapotaka kuwaponya Waisraeli, uovu wa watu wa Efraimu hufunuliwa, matendo mabaya ya Samaria hujitokeza. Wao huongozwa na udanganyifu, kwenye nyumba wezi huvunja nje barabarani wanyang'anyi huvamia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ninapotaka kumponya Isiraeli, ndipo, panapotokea wazi manza za Efuraimu na mabaya ya Samaria, kwani hutenda ya uwongo, nao wezi hujipenyeza nyumbani, nako nje huenea wanyang'anyi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakati nitakapo kumponya Israeli, ndipo yafunuliwapo maovu ya Efraimu, na ubaya wa Samaria; maana wanatenda uongo, na mwivi huvunja nyumba za watu, na kundi la wanyang’anyi hushambulia nje.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila mara nikitaka kurudishia watu wangu hali yao ya mbele, ninapotaka kuwaponyesha Waisraeli, uovu wa watu wa Efuraimu unafunuliwa, matendo mabaya ya Samaria yanajitokeza. Wao wanaongozwa na udanganyifu, mwizi anabomoa nyumba; inje katika barabara wanyanganyi wanashambulia.