Hosea 7:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watakapokwenda nitatandaza wavu wangu niwanase, nitawaangusha chini kama ndege wa angani; nitamwaadhibu kadiri ya ripoti ya maovu yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watakapoenda, nitatupa wavu wangu juu yao; nitawavuta chini waanguke kama ndege wa angani. Nitakaposikia wakikusanyika pamoja, nitawanasa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watakapokwenda nitatandika wavu wangu juu yao; nitawashusha kama ndege wa angani; nitawarudi, kama vile mkutano wao ulivyosikia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watakapokwenda nitatandaza wavu wangu niwanase, nitawaangusha chini kama ndege wa angani; nitamwaadhibu kadiri ya ripoti ya maovu yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati watakapokwenda, nitatupa wavu wangu juu yao; nitawavuta chini waanguke kama ndege wa angani. Nitakaposikia wakikusanyika pamoja, nitawanasa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati watakapokwenda, nitatupa wavu wangu juu yao; nitawavuta chini waanguke kama ndege wa angani. Nitakaposikia wakikusanyika pamoja, nitawanasa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watakapokwenda nitatandika wavu wangu juu yao; nitawashusha kama ndege wa angani; nitawarudi, kama vile mkutano wao ulivyosikia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watakapokwenda nitatandaza wavu wangu niwanase, nitawaangusha chini kama ndege wa angani; nitamwaadhibu kadiri ya ripoti ya maovu yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kila mara walipokwenda, niliwatandia wavu wangu, niwanase kama ndege wa angani, kisha nikawapatiliza, kama mkutano wao ulivyoambiwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watakapokwenda nitatandika wavu wangu juu yao; nitawashusha kama ndege wa angani; nitawarudi, kama vile mkutano wao ulivyosikia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watakapokwenda nitatandaza wavu wangu niwanase, nitawaangusha chini kama ndege toka katika anga; nitamwaazibu kufuatana na jinsi walivyotangaza kwa kusanyiko lao.