Hosea 7:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wote ni wazinzi; wao ni kama tanuri iliyowashwa moto ambao mwokaji hauchochei tangu akande unga mpaka mkate utakapoumuka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wote ni wazinzi, wanawaka kama tanuru ambalo moto wake mwokaji hana haja ya kuuchochea kuanzia kukanda unga hadi umekwisha kuumuka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hao wote ni wazinzi; wamekuwa kama tanuu iliyotiwa moto na mwokaji; huacha kuuchochea moto, tangu kuukanda unga hata umekwisha kutiwa chachu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wote ni wazinzi; wao ni kama tanuri iliyowashwa moto ambao mwokaji hauchochei tangu akande unga mpaka mkate utakapoumuka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wote ni wazinzi, wanawaka kama tanuru ambayo moto wake mwokaji hana haja ya kuuchochea kuanzia kukanda unga hadi umekwisha kuumuka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wote ni wazinzi, wanawaka kama tanuru ambayo moto wake mwokaji hana haja ya kuuchochea kuanzia kukanda unga hadi umekwisha kuumuka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hao wote ni wazinzi; wamekuwa kama tanuri iliyotiwa moto na mwokaji; asiyehitajika kuuchochea moto, tangu kuukanda unga hadi utakapokwisha kutiwa chachu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wote ni wazinzi; wao ni kama tanuri iliyowashwa moto ambao mwokaji hauchochei tangu akande unga mpaka mkate utakapoumuka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wao wote ni wazinzi, hufanana na jiko lililowashwa moto na mchoma mikate, naye akiisha kukanda unga, hupumzika kwa kuchochea moto, hata unga uwe umechachuka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hao wote ni wazinzi; wamekuwa kama tanuu iliyotiwa moto na mwokaji; huacha kuuchochea moto, tangu kuukanda unga hata umekwisha kutiwa chachu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wote ni wazinzi; wao ni kama furu iliyowashwa moto ambayo mutengenezaji wa mikate haichochei tangia wakati anapoponda unga mpaka mikate itakapovimba.