Hosea 8:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Walijiwekea wafalme bila kibali changu, walijiteulia viongozi ambao sikuwatambua. Wamejitengenezea miungu ya fedha na dhahabu, jambo ambalo litawaangamiza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wanaweka wafalme bila idhini yangu, wamechagua wakuu bila kibali changu. Kwa fedha zao na dhahabu wamejitengenezea sanamu kwa ajili ya maangamizi yao wenyewe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wamesimamisha wafalme, lakini si kwa shauri langu; wamejifanyia wakuu, lakini nalikuwa sina habari; kwa fedha yao na dhahabu yao wamejifanyizia sanamu, kusudi wakatiliwe mbali.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Walijiwekea wafalme bila kibali changu, walijiteulia viongozi ambao sikuwatambua. Wamejitengenezea miungu ya fedha na dhahabu, jambo ambalo litawaangamiza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wanaweka Wafalme bila idhini yangu, wamechagua wakuu bila kibali changu. Kwa fedha zao na dhahabu wamejitengenezea sanamu kwa ajili ya maangamizi yao wenyewe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wanaweka wafalme bila idhini yangu, wamechagua wakuu bila kibali changu. Kwa fedha zao na dhahabu wamejitengenezea sanamu kwa ajili ya maangamizi yao wenyewe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wamesimamisha wafalme, lakini si kwa shauri langu; wamejifanyia wakuu, lakini nilikuwa sina habari; kwa fedha yao na dhahabu yao wamejifanyia sanamu, kusudi wakatiliwe mbali.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Walijiwekea wafalme bila kibali changu, walijiteulia viongozi ambao sikuwatambua. Wamejitengenezea miungu ya fedha na dhahabu, jambo ambalo litawaangamiza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wameweka wafalme, nisiowaagiza mimi, wakaweka wakuu, nisiowajua! Kwa fedha zao na kwa dhahabu zao wakajitengenezea vinyago, kusudi viangamizwe tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wamesimamisha wafalme, lakini si kwa shauri langu; wamejifanyia wakuu, lakini nalikuwa sina habari; kwa fedha yao na dhahabu yao wamejifanyizia sanamu, kusudi wakatiliwe mbali.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walijiwekea wafalme bila ruhusa yangu, walijichagulia wakubwa ambao sikuwatambua. Wamejitengenezea miungu ya feza na zahabu, jambo ambalo litawaangamiza.