Hosea 8:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wa Samaria, naichukia sanamu yenu ya ndama. Hasira yangu inawaka dhidi yenu. Mtaendelea mpaka lini kuwa na hatia?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ee Samaria, tupilieni mbali sanamu yenu ya ndama! Hasira yangu inawaka dhidi yao. Watakuwa najisi hadi lini?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Amemtupa ndama yako, Ee Samaria; hasira yangu imewaka juu yao; siku ngapi zitapita kabla ya hao kupata hali isiyo na hatia?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wa Samaria, naichukia sanamu yenu ya ndama. Hasira yangu inawaka dhidi yenu. Mtaendelea mpaka lini kuwa na hatia?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ee Samaria, tupilieni mbali sanamu yenu ya ndama! Hasira yangu inawaka dhidi yao. Watakuwa najisi mpaka lini?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ee Samaria, tupilieni mbali sanamu yenu ya ndama! Hasira yangu inawaka dhidi yao. Watakuwa najisi mpaka lini?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndama wako amemtupa, Ee Samaria; ghadhabu yangu imewaka juu yao; Wataendelea kuwa na hatia hadi lini?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wa Samaria, naichukia sanamu yenu ya ndama. Hasira yangu inawaka dhidi yenu. Mtaendelea mpaka lini kuwa na hatia?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndama yako, Samaria, nimeitupa, makali yangu yakapata kuwaka kwa ajili yao. Mpaka lini wataweza kuendelea hivyo pasipo kutakaswa?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Amemtupa ndama yako, Ee Samaria; hasira yangu imewaka juu yao; siku ngapi zitapita kabla ya hao kupata hali isiyo na hatia?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Enyi watu wa Samaria, ninaichukia sanamu yenu ya mwana-ngombe. Hasira yangu inawaka juu yenu. Mutaendelea kuwa na makosa mpaka wakati gani?