Hosea 9:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku za adhabu zimewadia, naam, siku za kulipiza kisasi zimefika; Waisraeli lazima wautambue wakati huo! Nyinyi mnasema, “Nabii ni mpumbavu; anayeongozwa na roho ni mwendawazimu.” Mnasema hivyo kwa sababu ya uovu wenu mkubwa, kwa sababu ya chuki yenu kali dhidi yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku za adhabu zinakuja, siku za malipo zimewadia. Israeli na afahamu hili. Kwa sababu dhambi zenu ni nyingi sana na uadui wenu ni mkubwa sana, nabii anadhaniwa ni mpumbavu, mtu aliyeongozwa na Mungu anaonekana mwendawazimu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Siku za kupatilizwa zimekuja, siku za kulipa zimefika; Israeli atayajua hayo; huyo nabii ni mpumbavu, huyo mtu mwenye roho ana wazimu; kwa sababu ya wingi wa uovu wako, na kwa sababu uadui umekuwa mkubwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku za adhabu zimewadia, naam, siku za kulipiza kisasi zimefika; Waisraeli lazima wautambue wakati huo! Nyinyi mnasema, “Nabii ni mpumbavu; anayeongozwa na roho ni mwendawazimu.” Mnasema hivyo kwa sababu ya uovu wenu mkubwa, kwa sababu ya chuki yenu kali dhidi yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku za adhabu zinakuja, siku za malipo zimewadia. Israeli na afahamu hili. Kwa sababu dhambi zenu ni nyingi sana na uadui wenu ni mkubwa sana, nabii anadhaniwa ni mpumbavu, mtu aliyeongozwa na Mungu anaonekana mwenda wazimu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku za adhabu zinakuja, siku za malipo zimewadia. Israeli na afahamu hili. Kwa sababu dhambi zenu ni nyingi sana na uadui wenu ni mkubwa sana, nabii anadhaniwa ni mpumbavu, mtu aliyeongozwa na Mungu anaonekana mwendawazimu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Siku za kupatilizwa zimekuja, siku za kulipa zimefika; Israeli atayajua hayo; huyo nabii ni mpumbavu, huyo mtu mwenye roho ana wazimu; kwa sababu ya wingi wa uovu wako, na kwa sababu uadui umekuwa mkubwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku za adhabu zimewadia, naam, siku za kulipiza kisasi zimefika; Waisraeli lazima wautambue wakati huo! Nyinyi mnasema, “Nabii ni mpumbavu; anayeongozwa na roho ni mwendawazimu.” Mnasema hivyo kwa sababu ya uovu wenu mkubwa, kwa sababu ya chuki yenu kali dhidi yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku za mapatilizo zitafika! Siku za malipizi zitafika! Ndipo, Waisiraeli watakapojua, kama mfumbuaji ni mpumbavu, kama mtu wa kiroho ni mwenye wazimu, kwani manza, ulizozikora, ni nyingi, nao upingani wako ni mwingi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Siku za kupatilizwa zimekuja, siku za kulipa zimefika; Israeli atayajua hayo; huyo nabii ni mpumbavu, huyo mtu mwenye roho ana wazimu; kwa sababu ya wingi wa uovu wako, na kwa sababu uadui umekuwa mkubwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku za azabu zimetimia, siku za kulipiza kisasi zimefika; Waisraeli lazima wautambue wakati huo! Ninyi munasema: Nabii ni mupumbafu; anayeongozwa na roho ni mwenda-wazimu. Munasema hivyo kwa sababu ya uovu wenu mukubwa, kwa sababu ya chuki yenu kali juu yake.