Isaiah 1:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Msiniletee tena matoleo yenu yasiyo na maana; ubani ni chukizo kwangu. Acheni kufanya sikukuu za mwezi mpya, Sabato na mikutano mikubwa ya ibada; sikubali ibada zilizochanganyika na dhambi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Acheni kuniletea sadaka zisizokuwa na maana! Uvumba wenu ni chukizo kwangu. Miandamo ya Mwezi, Sabato na makusanyiko ya ibada: siwezi kuvumilia makusanyiko yenu maovu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Msilete tena matoleo ya ubatili; uvumba ni chukizo kwangu; mwezi mpya na sabato, kuita makutano; siyawezi maovu hayo na makutano ya ibada.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Msiniletee tena matoleo yenu yasiyo na maana; ubani ni chukizo kwangu. Acheni kufanya sikukuu za mwezi mpya, Sabato na mikutano mikubwa ya ibada; sikubali ibada zilizochanganyika na dhambi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Acheni kuniletea sadaka zisizokuwa na maana! Uvumba wenu ni chukizo kwangu. Miandamo ya Mwezi, Sabato na makusanyiko ya ibada: siwezi kuvumilia makusanyiko yenu maovu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Acheni kuniletea sadaka zisizokuwa na maana! Uvumba wenu ni chukizo kwangu. Miandamo ya Mwezi, Sabato na makusanyiko ya ibada: siwezi kuvumilia makusanyiko yenu maovu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Msilete tena matoleo ya ubatili; uvumba ni chukizo kwangu; mwezi mwandamo na sabato, kuita makutano; siyawezi maovu hayo na makutano ya ibada.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Msiniletee tena matoleo yenu yasiyo na maana; ubani ni chukizo kwangu. Acheni kufanya sikukuu za mwezi mpya, Sabato na mikutano mikubwa ya ibada; sikubali ibada zilizochanganyika na dhambi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Acheni kuleta tena vilaji vya tambiko visivyofaa! Uvumba nao hunitapisha, hata sikukuu za miandamo ya mwezi nazo za mapumziko na za makusanyiko; sivumilii, upotovu ukiwa hapohapo, mnaponikusanyikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Msilete tena matoleo ya ubatili; uvumba ni chukizo kwangu; mwezi mpya na sabato, kuita makutano; siyawezi maovu hayo na makutano ya ibada.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musiniletee tena matoleo yenu yasiyokuwa na maana; ninachukizwa na sadaka yenu ya ubani. Muache kufanya sikukuu za mwandamo wa mwezi, Sabato na mikutano ya ibada; sikubali ibada zilizochanganyika na maovu.