Isaiah 1:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Njoni, basi, tuhojiane. Ingawa mna madoa mekundu ya dhambi, mtatakaswa na kuwa weupe kama theluji; madoa yenu yajapokuwa mekundu kama damu, mtakuwa weupe kama sufu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Njooni basi tujadiliane,” asema Mwenyezi Mungu. “Ingawa dhambi zenu ni kama rangi nyekundu, zitakuwa nyeupe kama theluji; ingawa ni nyekundu sana kama damu, zitakuwa nyeupe kama sufu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Njoni, basi, tuhojiane. Ingawa mna madoa mekundu ya dhambi, mtatakaswa na kuwa weupe kama theluji; madoa yenu yajapokuwa mekundu kama damu, mtakuwa weupe kama sufu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Njoni basi na tuhojiane,” asema BWANA. “Ingawa dhambi zenu ni kama rangi nyekundu, zitakuwa nyeupe kama theluji; ingawa ni nyekundu sana kama damu, zitakuwa nyeupe kama sufu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Njooni basi tuhojiane,” asema bwana. “Ingawa dhambi zenu ni kama rangi nyekundu, zitakuwa nyeupe kama theluji; ingawa ni nyekundu sana kama damu, zitakuwa nyeupe kama sufu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama damu, zitakuwa kama sufu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Njoni, basi, tuhojiane. Ingawa mna madoa mekundu ya dhambi, mtatakaswa na kuwa weupe kama theluji; madoa yenu yajapokuwa mekundu kama damu, mtakuwa weupe kama sufu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Njoni, tuumbuane! Ndivyo, asemavyo Bwana. Makosa yenu ijapo yawe mekundu kama damu, yatakuwa meupe kama chokaa juani; ijapo yawe mekundu kama nguo za kifalme, yatakuwa kama pamba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe anasema hivi: Mukuje basi, tukate shauri. Zambi zenu zikionekana kuwa nyekundu, zitakuwa nyeupe kama teluji; zikionekana kuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama sufu.